JINSI FC BARCELONA ILIVYOIFUMUA ARSENAL, LIONEL MESSI AVUNJA REKODI,HAPA KUNA VIDEO AKIFUNGA MAGOLIUsiku wa February 23 klabu ya FC Barcelona ya Hispania ilikuwa imesafiri kutoka Hispania hadi London Uingereza kukutana na Arsenal katika mchezo wao wa kwanza wa michuano ya klabu Bingwa barani Afrika, mchezo ambao ulikuwa wa hatua ya 16 bora, hivyo kila timu ilikuwa inahitaji ushindi.
Mchezo ulimalizika kwa Lionel Messi kuipatia FC Barcelona ushindi wa goli 2-0, magoli ya Lionel Messi yaliofungwa dakika ya 71 na 83, yalifanya mitaa mbalimbali ya London Uingereza kupooza, kwani ndio makazi ya mashabiki wengi wa Arsenal.

Kwa matokeo hayo Arsenal italazimika kwenda Nou Camp kusaka ushindi wa zaidi ya goli mbili ili iweze kuiondoa FC Barcelona na wao watinge robo fainali. Hata hivyo ushindi wa goli mbili kwa Lionel Messi dhidi ya kipa wa Arsenal Petr Cech, unavunja mwiko wa Messi kutowahi kumfunga Petr Cech kwa jumla ya muda wa masaa 10 na dakika 11.

Kama hukupata nafasi ya kucheki mechi hii ndio video ya magoli ya Lionel Messi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post