HII NDIYO KAULI YA LOWASSA LEO KUHUSU UCHAGUZI WA MARUDIO ZANZIBAR



Aliyekuwa mgombea wa nafasi ya urais akiungwa mkono na vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananch UKAWA, Mh. Edwrad Lowassa amesema ni vema serikali ikahakikisha inapata suluhu ya mgogoro wa kisiasa visiwani Zanzibar kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa marudio machi 20 mwaka huu.
 
Mh. Edward Lowassa amesema hayo ofisini kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam wakati wa kikao chake na wazee kutoka chama cha Chadema ambapo amesema anaunga mkono uongozi wa CUF kutokushiriki uchaguzi huo huku akisisitiza endapo serikali ikishindwa kumaliza mgogoro huo kabla ya mach 20 huenda hali ya kisiasa Zanzibar ikabadilika.

Aidha amewahakikishia wazee hao kuwa yeye na uongozi mzima wa UKAWA wako imara katika kuhakikisha wanatetea maslahi ya watanaznia ambapo pia amemshukuru waziri mkuu kwa kuruhusu mikutano suala ambalo linawapa fursa ya kuajipanga ili kuwashukuru watanzania waliojitokeza kupiga kura mapema 25 ,huku pia akiigusia katiba ya Tanzania.

Kwa mujibu wa risala ya wazee hao iliyosomwa na mzee Enec Ngombare wamempongeza Mh. Lowassa kwa na uvumilivu wake baada ya uchaguzi ambapo pia wamemhakikishia kuwa wako pamoja nae katika safari ya kuelekea mwaka 2020.

Katika mkutano huo pia uliohudhuliwa na kada wa siku nyingi Kingune Ngombare Mwiru, Mh Lowassa amewataka wazanzibar na watanzania kwa ujumla kuwa watulivu na kuhakikisha wanadumisha amani ya nchi hasa katika kipindi hiki ambacho viongozi wanaendelea na juhudi za kutafuta suluhu ya kisiasa visiwani Zanzibar.
Via>>ITV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527