RAIS MAGUFULI: MAMBO YANAYOFANYIKA NDANI YA SERIKALI NI YA AJABU,MAHAKIMU NAO WATUMBULIWE MAJIPU TU



Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amemtaka jaji Mkuu wa Tanzania kutumbua majipu kwa kuwafukuza kazi mahakimu wote walioshindwa kufikia masharti yaliyowekwa ya kutoa hukumu 260 kwa mwaka kwa kuwa wanachangia kuondoa sifa ya nzuri ya mahakama. 
 
Akizungumza katika sherehe za uzinduzi wa mwaka mpya wa mahakama, Dkt Magufuli amesema bila ya kuchukua hatua hakuna kitakachofanyika kwa kuwa mambo yanayofanyika ndani ya serikali ni ya ajabu na yanaondoa sifa ya taifa la Tanzania.

Amezungumzia pia suala viongozi wa serikali na taasisi za serikali wanavyofanya ufisadi wa fedha za walipa kodi Dkt Magufuli kuwa nao lazima wawajibishwe.

Kuhusu udhaifu uliopo kwa upande wa ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka -DPPO- rais Dkt John Pombe Magufuli amesema haiwezekani mtuhumiwa anakamatwa na kidhibiti mikononi na kesi inachukua miaka kwa madai ya uchunguzi kutokamilika.

Kwa upande wake jaji mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Othumani Chande amesema mahakama inatarajia kuanza kusikiliza kesi za uchaguzi wa madiwani na wabunge kuanzia Februari 22 mwaka huu ambapo mashauri 221 ya kupinga matokeo ya uchaguzi yasikilizwa na jumla ya shilingi bilioni 3 zinahitajika, ambapo pia amesema mahakama iko katika mchakato wa kuanzisha mahakama maalum ya wahujumu uchumi na mafisadi.
Via>>>>ITV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527