Habari Njema!! TIGO YAWAPA WATEJA WAKE HUDUMA YA WHATSAPP BURE KABISA, ANGALIA HAPA JINSI YA KUPATA




Meneja Mkuu wa Kampuni ya Simu ya Tigo, Diego Gutierrez akizungumza na waandishi wa habari na wageni waalikwa mbalimbali wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo uliofanyika jana Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam




Wafanyakazi wa Tigo na wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakifurahia jambo wa uzinduzi wa huduma ya whatsapp bure kwa wateja wa tigo iliyofanyika jana katika hotel ya Hyatt Regency Jijini Dar es salaam




Hapa kila mgeni mualikwa akiwa busy na simu yake kwenye uzinduzi huo.




Ni kama wanasema 'tumependeza sana ngoja tujipige picha' wakati wa uzinduzi wa huduma ya whatsapp bure kwa wateja wa tigo iliyofanyika jana katika hotel ya Hyatt Regency Jijini Dar es salaam




Wageni waaalikwa wakiwa katika maski za " Emojis " wakifurahia jambo kwenye uzinduzi huduma ya whatsapp bure kwa wateja wa tigo iliyofanyika jana katika hotel ya Hyatt Regency Jijini Dar es salaam




Hapa ni furaha tupu kwa wanahabari.




Washereheshaji katika uzinduzi huo,Mc Taji Liundi na Mc Abby wakitoa maelezo jinsi gani wateja wa Tigo watakavyofurahia huduma ya whatsapp bure




Burudani ikiendelea kutoka kwa wasanii wa kikundi maalum cha maonesho ya jukwaa wakati wa uzinduzi wa huduma ya whatsapp bure kwa wateja wa tigo iliyofanyika jana katika hotel ya Hyatt Regency Jijini Dar es salaam.




Meneja Mkuu wa Kampuni ya Simu ya Tigo, Diego Gutierrez (katikati), akiwa na viongozi wenzake kutoka tigo katika maski za "Emojis " wakati wa uzinduzi wa huduma ya whatsapp bure kwa wateja wa tigo iliyofanyika jana katika hotel ya Hyatt Regency Jijini Dar es salaam




Meneja Mkuu wa Kampuni ya Simu ya Tigo, Diego Gutierrez (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na washereheshaji MC Taji Liundi na MC Abby wakati wa uzinduzi wa huduma ya whatsapp bure kwa wateja wa tigo iliyofanyika jana katika hotel ya Hyatt Regency Jijini Dar es salaam










Ofisa Mkuu wa Biashara wa Tigo, Shavkat Berdiev (kushoto ) Meneja wa gharama wa Tigo Jakhangic Tulaganov na Meneja masoko Olivier prentout wakifurahia jambo wakati wa uzinduzi wa huduma ya whatsapp bure kwa wateja wa tigo iliyofanyika jana katika hotel ya Hyatt Regency




Bloggers wakiwa katika picha ya pamoja na msanii Lucas Muhuvile 'Joti' wakati wa uzinduzi wa huduma ya whatsapp bure kwa wateja wa tigo iliyofanyika jana katika hotel ya Hyatt Regency Dar esSalaam, Februari 2, 2016- Kampuni ya Tigo Tanzania ambayo inaongoza kwa mtindo wa maisha ya kidijitali imetangaza huduma ya bure ya WhatsApp kwa watumiaji wa huduma hiyo ikiwa ni mara ya kwanza kwa kampuni
ya simu kutoa ofa ya bure ya mtandao huo wa jamii nchini.


Akitangaza upatikanaji bure wa huduma hiyo kwa vyombo vya habarijijini Dar es Salaam, Meneja Mkuu wa
Tigo Diego Gutierrez amesema kuwa wateja wote wa Tigo wanaotumia vifurushi vya intaneti vya
kampuni hiyo kwa wiki na mwezi watapata huduma
ya WhatsApp bure. Tigo ina wateja zaidi ya milioni 10.


Huduma ya WhatsApp ambayo ni maarufu kwenye kutuma ujumbe kwa njia ya simu, ina watumiaji zaidi ya milioni nane nchini Tanzania  na duniani inatumiwa na watu wapatao milioni 900.
WhatsApp inawezesha watumiaji  kubadilishana habari, ujumbe, video na miito ya sauti.


“Kuanzia sasa na kuendelea wateja wote wa Tigo wanaonunua
vifurushi vyetu vya wiki au mwezi watakuwa na fursa ya kufurahia WhatsApp BURE. Hili linawezekana kama mteja ana smartphone. Huduma ya bure ya WhatsApp kwa wateja wetu inaonesha jinsi
tulivyojikita katika kuboresha mabadiliko kwenye maisha ya kidijitali na hivyo kuongoza kwenye kutoa teknolojia ya
hali ya juu pamoja na ubunifu”, alisema Gutierrez.


Kwa Mujibu wa Gutierrez, ili kufurahia huduma hii, jambo analohitaji mteja wa Tigo ni kuwa na  kifurushi cha intaneti cha wiki au mwezi ambacho anaweza kukipata
kupitia *148*00# à Tigo-Tigo Xtreme/MiniKabangà Wiki au Mwezi + WHATSAPP YA
BURE. Huduma hii inapatikana kwa wanaomiliki simu za aina ya Blackberry, Android na Nokia Symbian60.


WhatsApp ni huduma dada na huduma huduma Facebook ambayo
iliingia makubaliano na Tigo mwaka 2014 na kuwapa fursa wateja wa Tigo hudumaya Facebook bure na kwa lugha ya Kiswahili kupitia simu zao.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments