Makubwa Haya!! PICHA YA KIAZI YAUZWA DOLA MILIONI MOJA,ILIKUWA UKUTANI JAMAA AKAITAMANI



Sio jambo la ajabu kutamani kula viazi hususan baada ya kubugia glasi kadha ya mvinyo.

Iwe ni viazi karai ,viazi vya kuchoma au hata Chips lakini bwana mmoja nchini Uingereza ameustaajabisha ulimwengu kwa kununua picha ya kiazi kwa dola milioni moja.

Baada ya kumimina glasi kadhaa za kinywaji chake alitia sahihi hundi ya pauni laki saba u nusu £750,000 sawa na dola dola milioni moja za Marekani $1066199.97.

Mpiga picha Kevin Abosch aliiambia jarida la The Sunday Times

''sio mara ya kwanza kwa mtu aliyebugia kileo chake kununua picha aliyoiangalia ukutani''

''tulikuwa tumekunywa glasi mbili za mvinyo,,nilifurahi sana.'

''Lakini baada ya glasi zingine mbili za mvinyo bwana huyo alinisisitizia kuwa ,kwa kweli naipenda sana picha hiyo sijui iwapo unaweza kuniuzia hiyo''



''Baada ya majuma mawili tulikubaliana bei yake na malipo yakafanywa''

Abosch aliipiga picha kiazi hicho kutoka ulaya mwaka wa 2010 kama mojawapo ya msururu wa viazi asilia.

Alipata umaarufu mkubwa kwa kuwapiga picha wasanii maarufu Johnny Depp na muigizaji na mtayarishaji nyota Steven Spielberg.

Bei ya picha zake huwa ni takriban dola 285,00 au pauni £200,000.

Picha hiyo iliambatana na viazi asilia na mboga .
Via>>BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527