Kimenuka!! WENYEVITI WA MITAA WAZUA BALAA MANISPAA YA SHINYANGA,WAKOMAA NA MKURUGENZI,HASIRA ZAO ZATULIZWA KIAINA

Aliyesimama ni mwenyekiti wa wenyeviti wa mitaa,vijiji na vitongoji katika manispaa ya Shinyanga bwana Nassoro Warioba akifungua kikao cha wenyeviti hao leo katika shule ya msingi Town iliyopo mjini Shinyanga-Habari kamili iko chini baada ya picha zote...Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Mmoja wa wenyeviti hao akizungumza katika kikao hicho


Mmoja wa wenyeviti hao akizungumza katika kikao hicho


Katibu wa wenyeviti wa mitaa,vitongoji na vijiji katika manispaa ya Shinyanga Chief Abdalah Sube akitoa taarifa kwa wajumbe wa kikao hicho kuhusu yaliyojiri baada ya kukutana na mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Lewis Kalinjuna juu ya maombi/mapendekezo ya wenyeviti hao

Katibu wa wenyeviti wa mitaa,vitongoji na vijiji katika manispaa ya Shinyanga Chief Abdalah Sube akitoa taarifa kwa wajumbe wa kikao hicho kuhusu yaliyojiri baada ya kukutana na mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Lewis Kalinjuna juu ya maombi/mapendekezo ya wenyeviti haoMmoja wa wenyeviti hao akizungumza katika kikao hicho
Kaimu mkurugenzi wa manispaa hiyo Mwanamsiu Dosi ambaye ni afisa maendeleo ya jamii wa manispaa


Mwenyekiti na katibu wa Wenyeviti wa mitaa,vijiji na vitongoji katika manispaa ya Shinyanga (Nassoro Warioba Chief Abdalah Sube)wakiwa katika kikao hichoBaadhi ya Wenyeviti wa mitaa,vijiji na vitongoji katika manispaa ya Shinyanga wakiwa katika kikao hicho


Baadhi ya Wenyeviti wa mitaa,vijiji na vitongoji katika manispaa ya Shinyanga wakiwa katika kikao hicho wakifuatilia kilichokuwa kinaendeleaBaadhi ya Wenyeviti wa mitaa,vijiji na vitongoji katika manispaa ya Shinyanga wakiwa katika kikao hicho

Baadhi ya Wenyeviti wa mitaa,vijiji na vitongoji katika manispaa ya Shinyanga wakiwa katika kikao hicho

Aliyesimama ni mwenyekiti wa wenyeviti wa mitaa,vijiji na vitongoji katika manispaa ya Shinyanga bwana Nassoro Warioba akifunga kikao

Katibu  wa wenyeviti wa mitaa,vijiji na vitongoji katika manispaa ya Shinyanga bwana Chifu Abdalah Sube akizungumza na waandishi wa habari baada ya kikao-Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

*******

Wenyeviti wa serikali ya mitaa,vijiji na vitongoji katika manispaa ya Shinyanga wamemlalamikia mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Lewis Kalinjuna kwa kupuuza maombi yao kuhusu kuboreshewa maslahi yao ikiwemo kuongezewa posho ya kila mwezi kutoka shilingi 15,000/= hadi 350,000/= kwa mwezi.

Wenyeviti hao wanaomba manispaa ya Shinyanga kuwapatia baiskeli kwa ajili ya kutekeleza vyema majukumu yao,kuwaongezea posho yao ya kila mwezi kutoka shilingi 15,000/= kwa mwezi hadi shilingi 350,000/= na kupewa kiinua mgongo cha shilingi milioni 8 kwa wenyeviti na shilingi milioni 2 kwa wajumbe wa serikali za mitaa,vijiji na vitongoji.

Akitoa taarifa katika kikao cha wenyeviti hao kilichofanyika leo latika shule ya msingi Town mjini Shinyanga,Katibu wa wenyeviti wa mitaa,vijiji na vitongoji katika manispaa hiyo Chifu Abdalah Sube alisema Desemba 27,2015 walifanya kikao na kukubaliana kupeleka mapendekezo kwa mkurugenzi lakini hawajaridhishwa na majibu yake.

“Baada ya kupeleka mapendekezo ya wajumbe wa kikao,mkurugenzi alisema serikali haiwezi kuongeza posho wala kiinua mgongo kwa wenyeviti mpaka waongeze uzalishaji katika mitaa,vijiji na vitongoji vyao,..kila anayeomba posho muulize anazalisha kiasi gani mtaani kwake na ameisaidiaje serikali,hapo ndipo atapata jibu la la namna gani asaidiwe”,alieleza Sube akinukuu maneno ya mkurugenzi.

“Kuhusu baiskeli mkurugenzi alisema wenyeviti wasisubiri baiskeli ili wazifanyie starehe,kwanza waifanyie kazi serikali ndipo hayo mambo wanayoyataka yafanyike...lakini pia alisema kuwa wenyeviti wasifanye vikao kujadili serikali... badala yake wawajibike ili kuhakikisha kuwa uzalishaji unaongezeka katika mitaa,vijiji na vitongoji ikiwemo kuongeza kasi ya ukusanyaji wa kodi za majengo na maduka”,alifafanua Sube.

Kufuatia hali hiyo wenyeviti hao walioonekana kutoridhishwa na majibu ya mkurugenzi wa manispaa hiyo,na kuiomba serikali ya awamu ya tano kuwajali kwani ndiyo wanafanya kazi kubwa zaidi katika jamii ukilinganisha na madiwani na wabunge.

“Haya majibu ya mkurugenzi yamejaa kejeli na ubabe,haiwezekani atoe majibu rahisi kama haya,sisi tunafanya kazi masaa 24,tunasuluhisha migogoro katika jamii wakati mwingine usiku wa manane,tunalisha chakula chetu hadi watu waliopotea ambao kimbilio lao ni kwa viongozi wa mitaa,bado posho yenyewe ni shilingi elfu 15,tunatumia karatasi lakini serikali hata haijui tunatoa wapi karatasi hizo,lazima tuthaminiwe”,walieleza wenyeviti hao.

“Wakati mwingine tuheshimiane basi,huyu mkurugenzi hatufai,bora hata wakurugenzi waliopita tunamshukuru Festo Kang’ombe na Jane Mutagurwa hawa walikuwa wanatusikiliza japo utekelezaji ulikuwa unasuasua,siku hizi mbali na madai yetu kutosikilizwa,watendaji wa manispaa wamekuwa wakivamia katika mitaa yetu,wanafanya kazi zao kisha kuondoka bila kuwataarifu viongozi wa serikali za mitaa”,waliongeza wenyeviti hao.

Wenyeviti hao walisema wanadai posho iongezwe kutokana na kazi nzito wanayofanya ikiwemo kuhakikisha ulinzi na usalama unakuwepo katika jamii ingawa wanaonekana kutothaminiwa na viongozi wa serikali.

“Sisi hatuna mishahara,hii kazi tunafanya kama sifa tu,hivi katika maisha ya sasa nani anaweza kuishi kwa shilingi elfu 15?,bado hata hiyo hailetwi kwa wakati,bado tunalisha wananchi wenye matatizo mbalimbali,wengine wanalala majumbani kwetu,tumeomba walau baiskeli badala ya pikipiki,tunaambiwa ni starehe,hii ni dharau”,walisema wenyeviti hao.

“Wenyeviti wa kamati za ulinzi na usalama katika nchi hii ni wane tu,ambao ni wenyeviti wa mitaa/vijiji/vitongoji,mkuu wa wilaya,mkuu wa mkoa na rais lakini tunaambiwa hadi tufanye uzalishaji ndipo tuongezwe posho na madai yetu mengine,hata hili la ulinzi na usalama hawalioni??,kwanza tulipaswa kuwa na posho kubwa kuliko hata madiwani na wabunge”,walieleza wenyeviti hao wa mitaa.

Katika hatua nyingine wenyeviti hao waliomba kupatiwa semina elekezi ili watekeleze vyema majukumu yao kwani hivi sasa wajumbe na wenyeviti wa serikali za mitaa,vijiji na vitongoji wanaingiliana kiutendaji huku wakiwataka watumishi wa manispaa kutovamia mitaani bila kutoa taarifa kwa viongozi wa serikali za mitaa.

Kwa upande wake mwenyekiti wa wenyeviti wa mitaa,vijiji na vitongoji katika manispaa ya Shinyanga Nassoro Warioba aliwataka viongozi wa serikali za mitaa kuendelea kushirikiana ili kupigania haki zao huku wakitimiza wajibu wao kwa wananchi ili kuendana na kauli mbiu ya serikali ya awamu ya tano ya “Hapa Kazi tu” kwa kinachotakiwa ni kuwaletea maendeleo wananchi.

Naye Kaimu mkurugenzi wa manispaa hiyo Mwanamsiu Dosi ambaye ni afisa maendeleo ya jamii wa manispaa hiyo aliyejitahidi kwa kiasi kikubwa kutuliza hasira za wenyeviti hao ,aliwaahidi wenyeviti hao kwenda kumshauri mkurugenzi wa manispaa hiyo Lewis Kalinjuna ili asikilize madai ya wenyeviti hao.

“Kwa jinsi hali ilivyo katika kikao hiki inaonesha hamjaridhishwa na majibu ya mkurugenzi,nitakaa naye nimshauri kwa yale yote yalijitokeza katika kikao hiki,lakini naomba tu niwaambie tu kuwa siyo mambo yote mnayoomba yanaweza kutekelezwa”,alisema Dosi.

Na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527