HII HAPA ORODHA YA RADIO 21 NA TV 6 ZILIZOFUNGWA NA TCRA TANZANIA,ZIMO ZA LOWASSA,DIALO NA CCM

Mamlaka ya Mawasiliano TCRA imevifungia vituo 21 vya Radio na 6 vya TV kikiwemo kituo cha Star TV, Radio free Afrika, Kiss Fm na Uhuru FM kwa kushindwa kulipa kodi ya lesseni kwa wakati ..


Akitangaza uamuzi huo, mkurugenzi wa habari na mawasiliano wa TCRA Innocent Mungy, amesema kuwa mitambo ya vituo hivyo itazimwa ifikapo leo Jumapili saa 6 usiku, na itawashwa baada ya vituo hivyo kulipa madeni yanayowakabili.


Mungy amesema mamlaka hiyo haiwezi kusema ni kiasi gani cha pesa ambacho vituo hivyo vinadaiwa kwa madai kuwa kanuni na taratibu haziwaruhusu kutaja kiasi hicho kwa kuwa ni siri kati ya TCRA na mteja.


Aidha Mungy amesema kuwa TCRA imewataka wadau wote wa mawasiliano nchini kutii sheria bila shuruti na kufuata taratibu, huku akisisitiza kuwa zoezi hilo la kuwasaka wanaokwepa kodi ni endelevu.

==> Vituo vingine vilivyofungiwa ni;

Sibuka FM
Breez FM
Country FM
Ebony FM
Hot FM
Impact FM
Iringa Municipal TV
Kiss FM
Kitulo FM
Kifimbo FM
Mbeya City Municipal TV
Radio 5
Radio Free Afrika (RFA)
Musa Television Network
Pride FM radio
Radio Huruma
Radio Uhuru
Star TV
Rock FM Radio
Standard FM radio
Sumbawanga Municipal TV
Tanga City TV
Top Radio FM limited

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post