ANGALIA PICHA KILELE CHA MAADHIMISHO YA MIAKA 52 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR


Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein akisalimiana naRais Mstaafu wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo katika killele cha sherehe za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kutimia miaka 52,zilizofanyika katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja,ambapo mgeni rasmi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.

Pichani kutoka kushoto Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi,Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein,Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Davis Mwamunyange wakiwa katika kilele cha Sherehe za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kutimia miaka 52 katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja zilizofanyika leo

Baadhi ya Wananchi na Maafisa mbali mbali wa Serikali wakiwa katika sherehe za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kutimia miaka 52,zilizofanyika leo katika Uwanja wa Amaani Studium Mjini Unguja

Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa akisalimiana na Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu wakati alipowasili katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja katika Kilele cha sherehe za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kutimia miaka 52,ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Davis Mwamunyange katika kilele cha Sherehe za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kutimia miaka 52 katika Uwanja wa Amaan Studium zilizofanyika leo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akisalimiana na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein katika kilele cha Sherehe za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kutimia miaka 52 katika Uwanja wa Amaan Studium zilizofanyika leo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwapungia mkono wananchi walioshiriki katika kilele cha Sherehe za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kutimia miaka 52 katika Uwanja wa Amaan Studium leo akiwa katika gari maalum


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiteremka katika gari maalum alilopanda wakati akiwasalimia wananchi katika kilele cha Sherehe za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kutimia miaka 52 katika Uwanja wa Amaan Studium leo.
[Picha na Ikulu.]

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527