Siku moja kabla ya kuapishwa kwa rais mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli baadhi ya wageni mashuhuri wameanza kuwasili nchini kushuhudia kuapishwa kwa rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kabla ya Alhamisi ya Novemba,052015 siku ambayo Tanzania inafungua ukurasa mpya wa kuwa na rais wa awamu ya tano sherehe zitakazofanyika kwenye uwanja wa uhuru jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wananchi na wageni mbalimbali.
Wageni mbalimbali maarufu wameendelea kuwasili kupitia uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mmojawapo ni muhubiri mashuhuri barani Afrika na duniani kwa ujumla TB Joshua anatua katika uwanja huo kushuhudia zoezi la kuapishwa kwa Dr Magufuli.
Mhubiri huyo TB Joshua amelakiwa na mwenyeji wake ambaye ni rais mteule wa awamu ya tano Dr John Pombe Magufuli akiambatana na familia yake pamoja na kusalimiana na baadhi ya wananchi waliojitokeza kumlaki kabla TB Joshua kuelekea Ikulu kukutana na rais anayemaliza muda wake Dr Jakaya Mrisho Kikwete.

Mara tu baada ya kutua uwanja wa Ndeghe wa Kimataifa wa Julius Nyerere, TB Joshua alikwenda Ikulu moja kwa moja kumsalimia Rais Jakaya Mrisho Kikwete kumsabahi na kumpongeza kwa kufanikisha uchaguzi mkuu kwa uhuru na amani, huku akiondoka madarakani akiwa mtu mwenye furaha.
TB Joshua amepongeza Rais Kikwete pia kwa kupata Dkt Magufuli kama mrithi wake, akimtaja Rais huyo mpya mteule kama Rais wa Tanzania wa Baraka na Fanaka tele katika awamu hii mpya.


Social Plugin