Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) Dk. Charles Msonge amesema pamoja na kesho kutangazwa siku ya mapumziko, lakini mitihani ya kidato cha nne itaendelea kama ratiba ilivyo, hivyo wanafunzi wasikose kwenda shuleni.
Kauli ya Katibu mtendaji wa NECTA imekuja baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kuamua na kuitangaza kesho, Alhamisi, Novemba 5, mwaka huu, 2015, kuwa Sikukuu na siku ya mapumziko.
Rais Kikwete amefanya uamuzi huo, ili kuwawezesha Watanzania kushiriki katika sherehe za kuhitimisha Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Nne na kuingizwa madarakani Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Via>>EATV
Social Plugin