News Alert!! HII HAPA NYINGINE KALI KUTOKA SERIKALI YA MAGUFULI...MARUFUKU KUCHAPICHA KADI ZA KRISMASI NA MWAKA MPYA



Serikali imeendelea na msimamo wake wa kupunguza matumizi yasiyo ya lazima, baada ya Rais Dk.Magufuli kuondoa safari za nje, mamilioni ya pesa kuokolewa katika uzinduzi wa Bunge sasa imepiga marufuku uchapishaji wa kadi za sikukuu ya Krismasi na mwaka mpya.

Katika taarifa yake Katibu mkuu kiongozi Ombeni Sefue amepiga marufuku utengenezaji na uchapishaji wa kadi za Krismass na mwaka mpya kwa gharama za Serikali mwaka huu.

Balozi Sefue ameelekeza kuwa yeyote anayetaka kutengeneza ama kuchapisha kadi hizo afanye kwa gharama zake mwenyewe.

Taarifa hiyo iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi wa mawasiliano Gerson Msigwa imesema fedha zilizopangwa kugharamia utengenezaji wa uchapishaji wa kadi hizo zitumike kupunguza madeni ambayo Wizara, idara na Taasis za umma zinadaiwa na wananchi waliotoa huduma na bidhaa kwao au zipelekwe katika matumizi mengine.

Taarifa hiyo ilisomeka hivi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527