ANGALIA PICHA 37- SHEREHE FUPI NA YA KUSHTUKIZA KUMUAGA MTANGAZAJI MAARUFU NCHINI TANZANIA RND "BOB RICH"



Novemba 12,2015 Kijana Richard Ndariro maarufu kwa jina la BOB RICH ama RND,ambaye ni mtangazaji maarufu wa Radio Faraja Fm Stereo ya Shinyanga ambaye huendesha vipindi mbalimbali kikiwemo kipindi cha Faraja Mamboleo na Michapo ya Jioni anatangaza rasmi kuachana na radio hiyo na kuendelea na shughuli zingine tofauti na utangazaji....Usiku huu imefanyika hafla fupi na ya kushtukiza iliyohudhuriwa na baadhi ya watangazaji wenzake,marafiki na baadhi ya wapendwa wake katika eneo la bwalo la Jeshi Kambarage mjini Shinyanga...Pichani ni keki iliyoandaliwa kwa ajili yake...Nimekuletea picha 37 kilichojiri....Tazama hapa chini


MC wa Hafla fupi na kushtukiza kumuaga Richard
Ndariro,,,bwana Faustine Kasala ambaye ni mtangazaji wa Radio Faraja Fm Stereo ya Shinyanga akizungumza wakati wa hafla hiyo fupi



Watangazaji wa radio Faraja na wageni waalikwa




Kulia ni mtuma salamu maarufu nchini Tanzania anajulikana kwa jina la Mr Timberland/Gavana wa Shytown akifuatiwa na Katibu wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga Stephen Wang'anyi aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo fupi ya kumuaga Richard
Ndariro(wa pili kutoka kushoto),anayefuatia ni Agnes Kambarage kutoka Radio Faraja




Kushoto ni mtangazaji wa Radio Faraja Veronica Natalis maarufu kwa jina la V2 ambaye anawakilisha radio DW




Mkurugenzi wa Mipancho Entertainment bwana Egam Dropper akiwa eneo la tukio




Kushoto ni mtangazaji wa Radio Faraja bwana Faustine Kasala




Keki



Richard
Ndariro akikata keki




Zoezi la kukata keki linaendelea




Bob Rich akimlisha keki mgeni rasmi Bwana Stephen Wang'anyi




Bob Rich akimlisha keki mkurugenzi msaidizi wa Radio Faraja bwana Anikazi Kumbemba




Bob Rich akimlisha keki Egam Dropper




Bob Rich akimlisha keki Faustine Kasala




Bob Rich akikumbatiana na mjukuu wake baada ya kumlisha keki




Bob Rich akimlisha keki Mtangazaji wa Radio Faraja Steve Kanyefu maarufu kwa jina la Mwanaporii




BOB RICH akilishwa keki




Mtuma salamu maarufu nchini Tanzania Mr Phone aka mzee wa Check akizungumza alivyomfahamu Bob Rich




Veronica Natalis akieleza jinsi BOB Rich alivyokuwa msaada Radio Faraja kwamba alikuwa mtu wa kujituma anayependa kazi na mbunifu katika vipindi mbalimbali vya radio




Hafla inaendelea




Mwanaporii..mtangazaji wa Radio Faraja akisimulia jinsi BOB Rich alivyokuwa anajituma katika kazi na kushauri pia kusaidia wengine




Veronica Natalis akimlilia BOB Rich




Bob Rich akiangalia zawadi zake




Mkurugenzi wa Mipancho Entertainment Egam Dropper aliyewakilisha wasanii wa Shinyanga akizungumza katika hafla hiyo fupi




Egam Dropper akisimulia jinsi Bob Rich alivyokuwa mwepesi wa kuchukua na kucheza radioni nyimbo za wasanii wa Shinyanga




Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari pia mkurugenzi wa Malunde1 blog bwana Kadama Malunde,ambaye amewahi kuwa mwandishi wa habari,Mtangazaji na Mhariri mkuu wa habari wa Radio Faraja akizungumza katika hafla hiyo ambapo alieleza jinsi BOB Rich alivyokuwa anajituma katika kazi na ubunifu wake katika kazi ya utangazaji




Mr Timberland/Gavana wa Shytown akisimulia jinsi Bob Rich alivyokuwa anathamini watuma salamu kwa njia ya Radio katika vipindi vyake




Veronica,Eliza na Agnes kutoka Radio Faraja wakiwa katika hafla hiyo




Mkurugenzi msaidizi wa radio Faraja Anikazi Kumbemba akizungumza katika halfa hiyo fupi na ya kushtukiza ambapo aliwataka watangazaji wengine kuiga mfano wa Bob Rich kwani ni kijana anayejituma,mwadilifu,mvumilifu na mbunifu




Mgeni rasmi Stephen Wang'anyi akizungumza katika hafla hiyo fupi na ya kushtukiza




Bob Rich akiwashukuru wafanya kazi wa Radio Faraja,wadau na marafiki zake na kudai kuwa sasa anaachana na kazi ya utangazaji na ataendelea na kazi nyingine tofauti na ya uandishi wa habari




Chakula cha pamoja nacho kilikuwepo....




Zoezi la kuchukua chakula likaendelea




Kila mshiriki alikula na kunywa




Tunakula pamoja baada ya kumuaga BOB Rich




Tunakula....



Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post