
Akiwa mjini Tarime Edward Lowasa alifanikiwa kuhutubia mikutano katika maeneo ya Salali,Nyamongo na mgumu kabla ya kuhitimisha kwa kuhutubia maelfu ya wakazi wa mji wa Tarime katika uwanja wa Sabasaba
Mgombea urais kupitia chama cha chadema anayeungwa mkono na vyama vinne vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi Ukawa Edward Lowasa ameahidi kuboresha mishahara ya walimu na kulipa stahiki zao zote kama watanzania watampa ridhaa kuwa rais wa nchi.

Baada ya kuhitimisha kwa kishindo kanda ya kaskazini sasa ni rasmi kanda ya ziwa akianzia Tarime mkoani Mara.
.jpg&container=blogger&gadget=a&rewriteMime=image%2F*)
Edward Lowasa anayetajwa kama mkombozi wa Tanzania ijayo, amesema ni dhamira yake kuona mtanzania akineemeka na keki ya taifa huku suala la elimu kwake akisema ndio itakuwa slaha kubwa ya kuifikisha Tanzania panapotakikana.
Fredrick Sumaye waziri mkuu mstaafu amesema wanatarime na watanzania kwa ujumla hawanabudi kuitumia vema Oct 25 kwa kukiondosha chama cha CCM kwani kuna kila dalili ya kuchokwa na watanzania.

Mhe. Edward Ngoyai Lowassa akiwasili Tarime mkoani Mara na kupokelewa na wananchi wa Tarime kwa shangwe,vifijo na nderemo wakiimba Rais...Rais...Rais..huku wakielekea kwenye uwanja mkutano wa 77 Tarime mjini leo Jumamosi 10/10/2015




"Tarime tunataka maji tumaini letu ni Lowassa" Leo Jumamosi 10/10/2015



Mhe. Edward Ngoyai akiwanadi wagombea udiwani Mugumu wilaya ya Serengeti leo Jumamosi 10/10/2015



Mgombea jimbo la Tarime mjini Ester Matiku akiongea na Wanatarime leo, katika viwanja vya 77 Tarime mjini, tarehe 10/10/2015

Edward Ngoyai Lowassa akiongea na wananchi wa Tarime mjini katika viwanja vya 77 leo Jumamosi 10/10/2015




Nyamongo na Sirari







Social Plugin