Mgombea mwenza urais kupitia Chama Cha Mapinduzi Mheshimiwa Samia Suluhu leo amekusanya maelfu ya wakazi wa Shinyanga katika viwanja vya Shycom Mjini Shinyanga wakati wa kampeni za kumnadi mgombea urais wa CCM Dk John Pombe Magufuli,wabunge na madiwani wa CCM ili wapewe kura siku ya uchaguzi mkuu Oktoba 25 mwaka huu.
Akizungumza mjini Shinyanga mgombea mwenza wa urais kupitia CCM Samia Suluhu Hasani amewataka wakazi wa mkoa wa Shinyanga na wafanya biashara ndogondogo kukiamini kuwa kikifanikiwa kuingia madarakani katika awamu ya tano kitafanya mabadiliko makubwa kwa wafanyabiashara wadogo kuondoa za kero ushuru na kitawaunganisha na mifuko ya hifadhi ya jamii na taasisi zingine za fedha ili wapate mikopo isiyo na mashariti magumu.
Katika namna ya pekee Mheshimiwa Samia aliwaomba wakazi wa Shinyanga mjini kumpa kura mgombea ubunge wa jimbo la Shinyanga mjini Mheshimiwa Stephen Masele akidai kuwa ni kijana mchapakazi na kuwahakikishia kuwa atawaletea maendeleo wananchi wa jimbo hilo.
Malunde1 blog ilikuwepo uwanjani,mwandishi wetu Kadama Malunde ametuletea picha 28...Angalia hapa chini
Wanachama wa CCM na wananchi wa mkoa wa Shinyanga wakifuatilia kilichokuwa kinajiri uwanjani
Wakazi wa Shinyanga wakiwa katika viwanja vya Shycom,kulia ni mtoto akicheza wimbo wa "CCM Mbele kwa mbele"
Mheshimiwa Samia Suluhu akisamiliana na mgombea ubunge jimbo la Msalala mheshimiwa Ezekiel Maige wakati akiwasili katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga leo jioni
Mheshimiwa Samia Suluhu akisalimiana mgombea ubunge jimbo la Kishapu mheshimiwa Suleiman Nchambi
Mheshimiwa Samia Suluhu akiwapungia mkono wakazi wa Shinyanga wakati anawasili katika viwanja vya Shycom
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga akisalimiana na mheshimiwa Samia Suluhu
Awali wagombea ubunge wa majimbo ya mkoa wa Shinyanga kwa tiketi ya CCM na wakazi wa mkoa huo walifikisha kilio chao cha kodi za kero zinazo kusanywa na baadhi ya halmashauri na kudai ziathiri kipato huku baadhi ya wajumbe wa kamati ya kampeni wakidai kuwa kero hizo zitamalizwa mapema baada ya Dk Magufuli kuapishwa kwani watanzania tayari wameshafanya maamuzi.
Kulia ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akifuatiwa na kada maarufu wa CCM Gasper Kileo na mgombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini Stephen Masele
Viongozi mbalimbali wakiwa jukwaa kuu
Mgombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini mheshimiwa Stephen Masele akiwasalimia wakazi wa Shinyanga ambapo pamoja na mambo mengine alisema miongoni mwa vipaumbele vyake ni kuondoa kero ya ajira,maji,barabara na mambo mengine kadha wa kadha
Mheshimiwa Masele alitumia fursa hiyo pia kumwombea kura mheshimiwa Magufuli,wabunge na madiwani wa CCM huku akiwaomba wakazi wa Shinyanga kumpa kura nyingi ili awaletee maendeleo
Mgombea mwenza urais CCM Samia Suluhu akiwahutubia wakazi wa Shinyanga ambapo aliwaasa kuchagua wagombea wa CCM kwani ndiyo chama pekee cha kuwaletea maendeleo wananchi
Maelfu ya wakazi wa Shinyanga wakimsikilia mheshimiwa Samia Suluhu
Mkutano unaendelea
Mkutano unaendelea
Wananchi wakinyoosha mikono baada ya kuulizwa kama watachagua wagombea wa CCM
Mkutano unaendelea
Mheshimiwa Samia Suluhu akimpigia debe mgombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini Stephen Masele
Mkutano unaendelea
Mheshimiwa Samia Suluhu akimwombea kura mgombea udiwani kata ya Shinyanga mjini Gulam Hafidh Mukadam
Tunafuatilia kinachoendelea....
Mheshimiwa Samia Suluhu akiwaaga wagombea udiwani katika manispaa ya Shinyanga
Mkutano unaendelea
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga akiondoka baada ya mkutano kumalizika
Wafuasi wa CCM wakicheza kwa mbwembwe na mgombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini Stephen Masele baada ya mkutano kumalizika
Mheshimiwa Masele akisindikizwa kwa shangwe na wakazi wa Shinyanga baada ya mkutano
Tunafurahia........
Mheshimiwa Samia Suluhu akiondoka katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga baada ya mkutano kumalizika
Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog Shinyanga
Social Plugin