Baadhi ya vijana wakimshangilia kwa vifijo Ndugu Hassan Kaunje, Mgombea Ubunge kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi mara baada ya kumalizika kwa sherehe za uzinduzi rasmi wa kampeni hizo katika Wilaya ya Lindi Mjini tarehe 3.9.2015.
Na Magreth Kinabo –Maelezo,Lindi
MKE wa Rais Mama Salma Kikwete amewataka wananchi wa Jimbo la Lindi Mjini kuhakikisha kwamba wanapiga kura ya ndiyo kwa mgombea wa kiti cha urais,Dkt. John Magufuli , mgombea kiti cha Ubunge Hassan Kaunje na wagombea viti cha udiwani ili waweze kupata maendeleo.
Kauli hiyo imetolewa jana jioni na Mama Kikwete ,ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi(NEC) wa Wilaya Lindi ,wakati wa uzinduzi wa kampeni ya chama hicho ya wilaya hiyo ili iliyoambatana na uzinduzi wa Ilani ya CCM kwa lengo la kuinadi na kuwanadi wagombea hao iliyofanyika kwenye uwanja wa Fisi.
“Leo nimekuja kufanya kazi hii moja ya kuhakikisha mgombea wa kiti cha urais, anashinda akiwemo mgombea wa kiti cha ubunge na wagombea wa viti vya udiwani,” alisema Mama Kikwete huku akiinadi picha ya mgombea wa kiti cha urais na kumnadi mgombea wa kiti cha Ubunge na wagombea viti vya udiwani katika kata mbalimbali kupitia chama hicho.
Mama Kikwete aliongeza kwamba ikiwa kila mtu atatoka na kufanya kampeni ya nguvu jimbo hilo litapata kura ya ndiyo viti hivyo.
Alisema wananchi hao endapo watafanya hivyo ifikapo Oktoba 25, mwaka huu, watakuwa wamefanya kazi iliyokamilika na watapata maendeleo kwani amani inapatikana mahali ambapo kuna maendeleo.
Pia aliwataka wananchi hao kuhakikisha watunza kadi zao za kupigia kura, wasije wakapoteza nafasi hiyo muhimu.
Mama Kikwete aliwataka wananchi hao, kukipa chama hicho kura ya ndiyo kwa sababu kina ilani, ni chama makini na kinafanya kazi kwa mipango.
Akizungumzia kuhusu ilani ya chama hicho,Mama Kikwete alisema,ina mambo makubwa manne, ambayo ni kuondoa umasikini, kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira, kuendeleza vita ya kupambana na rushwa na ubadhirifu wa mali ya umma.
Katika uzinduzi huo, Mama Kikwete alimkabidhi vitendea kazi mgombea wa kiti cha Ubunge ,ambavyo ni Katiba ya CCM na ilani hiyo ili aweze kufanya kazi huku akishangiliwa na mamia ya watu walijitokeza uwanjani hapo wengi wao wakiwa ni vijana.
Kaisi na waliokuwa wagombea wenzake wa kiti cha Ubunge 10 wameungana ili kumwuunga mkono Kaunje, hatua ambayo ilipongenzwa na Mama Kikwete.
“ Kura zipotosha huwezi kuhama kwenda chama kingine, bali mnaungana na kuwa kitu kimoja ni maneno mazuri ya kuiga mfano,” alisisitiza Mama Kikwete.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM, mkoa wa Lindi, Mzee Ally Mtopa aliwakemea watu wanaosema kuwa chama hicho hakijafanya maendeleo, ambapo alisema mtu anayesema hivyo, sawa na kumdharau baba yake aliyempeleka shule
Social Plugin