Ajali Kahama!! BASI LA PEACE MAKER LAGONGA NA KUUWA DEREVA BODABODA HUKO MJINI KAHAMA




Mwendesha pikipiki aliyefahamika kwa jina la David Amoni umri (27) mkazi wa Nyasubi wilayani kahama mkoani Shinyanga amefariki dunia akiwa anapatiwa matibabu baada ya kugongwa na Basi la kampuni ya Peace Maker.


Mashuhuda wa tukio hilo wameiambia Kahama fm kuwa ajali hiyo imetokeaa leo saa 12 ya asubuhi katika eneo la Faraja kata ya Kahama mjini, ambapo dereva huyo wakati anajaribu kuingia katika barabara kuu ghafla aligongwa na basi hilo.


Kwa mujibu wa taarifa hiyo, basi hilo la Abiria aina ya scania lenye namba za usajili T 167 ARV, lilikuwa likiendeshwa na Bahati Masanja (47) mkazi wa mwanza.


Akizungumza na Kahama Fm kaimu mganga mfawidhi wa hospitali ya halmashauri ya mji wa Kahama Dkt.George Masasi amesema mtu huyo alipoteza maisha muda mfupi baada kufikishwa hospitalini wakati akipatiwa matibabu na madaktari.


Dk.Masasi amebainisha kuwa mtu  huyo amepoteza maisha baada ya kupata majeraha kichwani na mguu wa kulia kuvunjika hivyo kusababisha kuvuja damu nyingi ambayo zimesababisha kifo chake.


Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha amethibitisha kutoka kwa tukio hilo na kudai kuwa chanzo chake ni mwendo kasi wa madereva wote wawili, na kwamba dereva wa basi hilo amekimbia na wanaendelea kumtafuta.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post