Vituko Duniani !! JAMAA AZUA BALAA NA SIMU YAKE YENYE COVER LA BASTOLA,POLISI WAHAHA





Ni kawaida ukikutana na warembo siku hizi wamependeza wenyewe, na simu zao wanataka zipendeze vilevile, basi kuna cover za kila aina utawakuta nazo.. wengine midoli, wengine ni maua maua… wanaume ni kawaida pia ukakutana na jamaa ana cover inaonekana kama nguo ya kijeshi hivi.

Jamaa aliyeingia kwenye Headlines Taiwan kakutwa na cover ya simu ambayo imekaa kama Bastola hivi, Polisi wakamwita wakaanza kumhoji kuhusu hiyo kitu ambayo ilikuwa inaonekana ameichomeka kwenye mfuko wa nyuma!!



Baada ya mahojiano Polisi wakagundua kwamba hiyo ni cover ya simu, wakamwachia.

Siku chache zilizopita aina hii ya cover za simu iliingia kwenye headlines Marekani ambapo watu wa Usalama walisema silaha sio kitu cha kuleta nacho utani, wameshuhudia mabalaa mengi ya matumizi ya silaha kwa hiyo hawako tayari kuona cover hizi zinazagaa mitaani na watu wanatumia!


Chuck Schume, Senator wa New York.

“Zimeingizwa sokoni na watu wanavutiwa nazo sana, ila zilipaswa kuwekwa lebo ya ‘HATARI’… Leo hii tunasema kwamba bastola sio kitu cha mchezo”—Hii ni nukuu ya alichokisema Chuck Schume, Senator wa New York Marekani.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post