News Alert!! MSHAURI MKUU WA RAIS AUAWA KWA KUPIGWA RISASI,MWANDISHI WA HABARI ALIYEPIGA PICHA YAKE APIGWA




Watu waliokuwa na bunduki wamemuuwa mkuu wa usalama wa zamani wa Burundi na mshauri mkubwa wa Rais Pierre Nkurunziza.


Walioshuhudia tukio hilo wanasema Jeneral Adolphe Nshimirimana alikufa pale gari lake liliposhambuliwa katika mji mkuu, Bujumbura.

Umoja wa Ulaya umesema mauaji yake yamezidisha wasiwasi, na kwamba juhudi za upatanishi lazima zianze tena.

Burundi imepita katika miezi kadhaa ya ghasia baada ya Rais Nkurunziza kuwania na kushinda muhula wa tatu wa uongozi.

Inafikiriwa kuwa Jenerali Nshimirimana bado alikuwa na mchango mkubwa katika usalama, hata baada ya kutolewa kuwa mkuu wa usalama nchini Burundi.

Mwandishi wa habari wa Ufaransa ambaye alipiga picha za pahala jenerali huyo aliposhambuliwa, alikamatwa na kupigwa.

Via>>BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post