NAPE AFUNGUKA KUHUSU MAKADA WA CCM WAOHAMIA UKAWA..AWAITA OIL CHAFU... LAPTOP ZA MAGUFULI NA LOWASSA KUINUNUA CHADEMA
Nape Nnauye akionesha kitabu cha Ilani ya Uchaguzi ya CCM ambayo imepitishwa jana Agosti 13,2015 katika Mkutano wa Chama hicho uliofanyika jana mjini Dodoma na inatarajiwa kuzinduliwa Agosti 23,mwaka huu katika uzinduzi wa Kampeni.********
Chama cha Mapinduzi kimesema hakishtushwi na makada na viongozi wanaoendelea kukihama chama hicho na kujiunga na Chadema na kudai kuwa wanao ondoka wana sababu zao binafsi na kwamba hakuna kiongozi wa upinzani ambaye hakuanzia CCM hivyo ni hali ya kawaida kwa chama kikubwa kama hicho ambacho kina mtaji wa wanachama takribani milioni nane.

Katibu wa NEC, itikadi na uenezi wa CCM, Bw Nape Nnauye, amebainisha hayo wakati akitoa ufafanuazi wa masuala mbalimbali yanayokihusu chama hicho kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam ambapo amesema waliohama na watakaoendelea kuhama siyo jambo jipya kwani kuna viongozi wakubwa waliondoka huku akitolea mfano wa Maalim Seif na Agustino Mrema.

Nape amesema wanachama hao wanahama kwa mapenzi yao binafsi wengine wamehama kwa sababu ya kushindwa katika kura za maoni za chama.


Hiki ndio alichokijibu kuhusu wanaohama CCM >>> “Hakuna kiongozi wa upinzani ambaye ameanzisha upinzani hakuanzia CCM, hata hao wanaoondoka.. waliondoka na watakaoondoka wanafata mkumbo uleule wa wenzao… wengi wao wanaondoka kwa sababu ya matatizo yao binafsi” >>> Nape Nnauye.


Kwenye sentensi nyingine Nape Nnauye ameyasema haya >>>> “Hivi kweli mtu ambaye amejiandaa leo sio tu Prof. Lipumba hata Dk. Slaa wamejiandaa muda mrefu sana na wakapewa matumaini na chama chao halafu dakika ya mwisho anatoka jamaa anakinunua chama… Freeman ameuza CHADEMA amemuuzia Lowassa”


Aidha chama hicho kimekanusha taarifa zinazosambaa mitandaoni kuwa, mgombea urais wa CCM, Dk.John Magufuli, alitangaza kuwagawia komputa walimu wote nchini kwa madai kuwa jambo hilo lipo kwenye ilani ya mwaka ambapo kimesema taarifa hizo ni za uzushi na kwamba ilani ya uchaguzi ya chama hicho ilipitishwa juzi mkoani Dodoma na inatarajiwa kuzinduliwa Agosti 23 mwaka huu.


“Kuna kauli inayodaiwa kuwa yaJohn Magufuli inayodai kwamba atawanunulia Walimu kompyuta nchi nzima… Magufuli hajawahi kuzungumzia suala hilo popote, kuna watu wanajaribu kuitengenza na kujaribu kuonesha kuwa ameanza kampeni… muda wa kampeni bado, wakati huo ukifika tutayazungumza.. wanaojaribu kutengeneza habari za uongo waache” — Nape Nnauye.

SIKILIZA SAUTI HAPA NAPE AKIZUNGUMZA


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post