MTANGAZAJI WA RADIO FREE AFRICA KIJUKUU CHA BIBI K ASHINDA KURA ZA MAONI CHADEMA USHETU

Mwandishi wa habari na mtangaaji wa Radio Free Africa William Bundala (KIJUKUU CHA BIBI K) ameshinda kura za maoni katika nafasi ya Udiwani katika kata ya Ulowa jimbo la Ushetu.


Akitangaza matokeo hayo Msimamizi wa uchaguzi huo Sangoma amesema Bundala ameshinda nafasi hiyo kwa kupata kura 46 dhidi ya Wagombea wenzake Charles Bahati aliyepata kura 14 na Marco Matheo ambaye hakupata kura yoyote katika kinyang’anyiro hicho.


Kuelekea uchaguzi mkuu Bundala alitangaza nia ya Kugombea Ubunge katika jimbo la Ushetu na udiwani katika kata ya Ulowa huku akisimamia kauli mbiu yake kuwa “Tunahitaji mawazo na nguvu mpya za vijana kuleta mabadiriko ya maendeleo”.


Akiongea kwa njia ya simu akiwa jimboni Bundala amesema kuwa huu ni mwanzo na kuongeza kuwa kwa sasa anasubiri kura za maoni za ubunge ili kuchaguliwa kupeperusha bendera ya Chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.


Sambamba na hayo Bundala amesema kuwa Tanzania ilipofikia kwa sasa inahitaji viongozi wazalendo wenye uchungu na rasilimali za wananchi na siyo kiongozi mwenye uchu wa madaraka anayetaka uongozi kwa rushwa.


Kwa upande wao wagombea waliokuwa katika kinyang’anyiro hicho cha udiwani wamesema kuwa wameridhika na matokeo na kwamba lengo la CHADEMA ni moja kuleta mabadiriko katika jimbo la Ushetu na kata ya ulowa kwa Ujumla.


Kwa sasa Bundala anasubiri kura za maoni za Ubunge zinazotarajiwa kufanyika wiki ijayo huku akiwa katika kinyang’anyiro hicho na watia nia wengine wawili ambao ni Mabula Nkwabi na John Kitibu ambaye alipata kura 45 katika kura za maoni za jimbo la Kahama Mjini.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post