Hot News!! BAADA YA KUPIGWA "STOP" ZIARA ZA LOWASSA MTAANI,OMBI LA UKAWA KUFANYA MKUTANO JANGWANI JUMAMOSI HII LAKATALIWA




Jiji la Dar es Salaam wamemzuia Mgombea wa UKAWA, Edward Lowassa kuzindua kampeni yake kwenye viwanja vya Jangwani Jumamosi ya 29 Agosti, 2015.


Mwenyekiti Mwenza wa UKAWA, James Mbatia amesema jiji umewagomea kufanya uzinduzi huo Jangwani kwa madai kuwa tayari kuna mtu mwingine ambaye ameshalipia uwanja huo.


Mbatia anasema pamoja na kufanya juhudi za kuomba kutajiwa aliyelipia uwanja huo ili wazungumze naye, Jiji walikataa.

Mbatia anasema viongozi wengine wa UKAWA wanashughulikia suala hilo ikiwa pamoja na kumtaka Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Damian Lubuva kuingilia kati.
Chanzo-EATV

HABARI ZAIDI FUATILIA HAPA>>>>TAARIFA ZAIDI KUHUSU MKUTANO WA UKAWA

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527