Tukio la Ajabu Simiyu!! MAREHEMU AZIKWA NA KITANDA,GODORO MEZA,MABEGI,VYOMBO NA VITU VINGINE VINGI...TAZAMA PICHA HAPABaadhi ya vitu vilivyokutwa juu ya kaburi la MarehemuBaadhi ya wananchi wakishuhudia tukio hilo

Wakazi wa eneo hilo wakishangaa mizigo hiyo


Katika tukio lisilokuwa la kawaida ambalo limevuta umati mkubwa wa watu katika mji wa Bariadi mkoani Simiyu katika eneo la makaburi  ya Kidinda ni wananchi kukuta kwenye kaburi moja wapo kukiwa na vitu mbalimbali ikiwemo godoro,mabegi,viti,kitanda,meza,vyombo na thamani mbalimbali za ndani.

Mashuhuda waliobaini kuwepo kwa  tukio hilo wamesema inawezekana linatokana na  imani za kishirikina.

Wamesema walifika katika makaburi hayo kwa ajili ya kumsitiri ndugu yao aliyefariki lakini cha kushangaza wakaona juu ya moja ya makaburi kukiwa na vitu hivyo na kudai kuwa huenda marehemu alizikwa navyo.

"Sisi tulikuwa na msiba wetu..tukaja hapa makaburini kumzika ndugu yetu, ghafla tukaona juu ya kaburi jingine kuna vitu hivyo..inaonekana huyu marehemu alizikwa na vitu vyake vikaletwa hapa makaburini na kuwekwa juu ya kaburi lake",ameeleza mmoja wa mashuhuda aliyejitambulisha kwa jina la Stanslaus Rweyemamu.


Kufuatia taarifa hizo waandishi wa habari ikiwemo Malunde1 blog bila kupoteza muda walifika katika eneo la tukio na kukuta vitu hivyo vikiwa juu ya kaburi la marehemu, huku wahusika waliofanya hivyo wakiwa hawajulikani kutokana na wahusika wa msiba kutokujulikana.

Hata hivyo baada ya askari polisi kufika eneo la tukio walivichukua vitu hivyo na kuondoka navyo kituo cha polisi Bariadi .

Kamanda wa polisi Mkoani Simiyu  Gemini Mushy amethibitisha kuwepo kwa   tukio hilo na kwamba wanaendeela kufanya uchunguzi ili kubaini chanzo cha tukio hilo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post