ANGALIA PICHA_MBUNGE WA CHADEMA ANUSURIKA KUFA BAADA YA HELIKOPTA YAKE KUPOTEA KWENYE MAWINGU NA KUNASA KWENYE MTIHelkopta ikiwa imeanguka leo


Mbunge wa Arumeru Mashariki,mkoani Arusha Joshua Nassari akiwa na helkopta yake( Picha kutoka maktaba ya Malunde1 blog)


Mbunge wa Arumeru Mashariki,mkoani Arusha Joshua Nassari amepata ajali ya helkopta aliyokua anaitumia kufanya ziara katika jimbo lake.

Habari za awali tulizozipata ni kwamba mbunge huyo wa Chadema Joshua Nassari amenusurika kufa baada ya Helkopta aliyokuwa anaitumia kuanguka baada ya kunasa kwenye mti baada ya kupotea kwenye mawingu.


Aidha taarifa hizo zinaeleza kuwa Mbunge huyo kwa Tiketi ya Chadema, na rubani wake walitoka wakiwa wazima na wapo katika Hospitali ya Kanila la Kilutheri ya Selian ya jijini Arusha.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post