NIMEKUWEKEA HAPA HOTUBA YA MHESHIMIWA LOWASSA AKIHAMIA CHADEMA HUKU AKISISITIZA KUWA SAFARI YA MATUMAINI IKO PALE PALEHatimaye aliyekuwa mbunge wa Monduli kwa tiketi ya CCM Edward Lowassa amejiunga rasmi na chama cha demokrasia na maendeleo Chadema huku akisisitiza kuwa hahusiki kwa namna yoyote ile na sakata la Richmond.


Mwaka 1995 akihutubia mkutano mkuu wa CCM mjini Dodoma, baba wa taifa alisema miaka 25 baadaye moja ya vigogo wa CCM anakiri kwa kusema mabadiliko ya kweli yako ndani ya upinzani.

Lowassa ametoa kauli hiyo ambayo inavunja ukimya na minong'ono ya muda mrefu baada ya kukatwa katika harakati za kuwania nafasi ya urais ndani ya CCM, anasema alichokishuhudia Dodoma ni ubakaji wa demokrasia.

Toka mwaka 2008 alipojiuzulu nafasi ya uwaziri mkuu jinamizi la sakata la Richmond limekuwa likimuandama, anasema sasa inatosha.

Mwenyekiti wa Chadema akizungumza mara baada ya kuwakabidhi kadi za uanachama Edward na mke wake Bi Regina Lowasa anasema chama chake kimefanya maamuzi sahihi kumualika  Edward Lowassa.

Hafla hiyo ya kumkabidhi Lowasa kadi ya Chadema imefanyika jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na familia yake ikiwa ni pamoja na viongozi mbalimbali wa Ukawa.

Katika hotuba yake Lowassa ameongea mambo mengi sana, Lowassa kasema kuwa CCM sio baba yake wala mama yake hivyo haoni sababu ya kukihama chama hicho, Isikilize hotuba yake yote hapa chini


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post