News Alert!! BASI LA SABUNI EXPRESS LAGONGA GARI YA MASISTA,WATU WANNE WAFARIKI DUNIA


Watu wanne wafariki dunia hapo hapo na wengine kujeruhiwa mara baada ya basi la Sabuni Express linalofanya safarizake kutoka wilayani Karagwe kwenda Mwanza jijini kugongana uso kwa uso na gari ndogo aina ya landcrusezer iliyokuwa ikiwasafirisha mapadri kutoka Bukoba kuelekea Karagwe katika eneo la Bugorola wilayan Misenyi.



Ajali hiyo imetokea majira sambili asubuhi katika eneo la Bugorola wilayani Misenyi ambapo baadhi mashuhuda wa ajali hiyo wamesema ajali hiyo imetokea wakati Dereva wa gari ndogo aina ya landcruser alipokuwa akijaribu kulipita lori lililokuwa mbele yake na kisha kukutana uso kwa uso na basi la Sabuni Express lililokuwa na biria wapatao arobani na tano na kusabisha vifo vya watu wanne ambao ni mapadri wawili,Sister mmoja na mseminalisti mmoja wote walikuwa wakisafiri na gari hiyo kuelekea karagwe.

Baadhi ya abiria waliokuwa wakisafiri na basi hilo wamesema dereva wa basi alikuwa katika mwendo wa kawaida kutokana ukungu ulikuwa kuwa umetenda barabarani.

Kwa upande wake katibu wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Kagera Kiiza Kilwanila amesema wamepokea maiti nne pamoja na majeruhi kadhaa ambao sasa halizao zinaendelea vizuri.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post