WANANCHI WENYE HASIRA KALI WAVAMIA KITUO CHA POLISI NA KUKICHOMA MOTO BAADA YA MWANAFUNZI KUGONGWA GARI NA KUPOTEZA MAISHA



Jengo la polisi likiteketea kwa moto



Wanafunzi wa shule ya Msingi Bunju B wakiwa wamefunga barabara hiyo baada ya kugongwa kwa mwanafunzi Mwenzao aliyefahamika kwa jina la Omari na kufariki dunia leo hii.


Wananchi wanaodaiwa kuwa na hasira kali wamevamia kituo cha polisi cha Bunju jijini Dar es Salaam kwa kuvunja vitu mbalimbali ikiwemo magari yaliyoegeshwa katika eneo hilo kisha kukichoma moto kituo hicho baada ya kugongwa kwa mwanafunzi wa darasa la nne na kufa papo hapo katika barabara ya Bagamoyo.



Mwandishi wa habari hizi alifanikiwa kufika katika eneo la Bunju na kukuta msongamano mkubwa wa magari katika barabara ya Bagamoyo, hali iliyosababishwa baadhi ya wanafunzi kufunga barabara kwa kishinikiza kujengwa kwa matuta ili kupunguza ajali za mara kwa mara baada ya kufariki kwa mtoto Tabia Omary mwanafunzi wa darasa la nne shule ya msingi Bunju A.

Licha ya kuchomwa moto katika barabara ya Bagamoyo, baadhi ya magari yalishindwa kupita katika barabara hiyo wakihofia kuvunjwa na wananchi huku kutokana na umati mkubwa wa wananchi hao baadhi ya askari walilazimika kuondoka katika kituo hicho ili kuokoa maisha yao huku sehemu ya barabara ya Bagamoyo ikionekana wazi.

Wananchi hao licha ya kushindwa kupambanua kuwa kugongwa kwa mtoto huyo katika barabara ya Bagamoyo haihusiani na kituo cha polisi, waliamua kuvunja kituo hicho pamoja na magari yaliyoegeshwa katika eneo hilo na kuiba vitu mbalimbali ndani ya magari hayo bila woga na kisha kuchoma moto kituo hicho wakati kituo hicho kilijengwa kwa ajili ya kutoa msaada kwao.

Mwandishi wa habari hizi ameshuhudia wananchi hao wakichoma kituo hicho moto bila kufikiria madhara yake kwanza, ambapo baada ya askari polisi kuongeza nguvu waliamua kupiga risasi za moto hewani na mabomu ya mchozi ili kutawanya wananchi hao huku baadhi ya kina mama nao wakiangua kilio baada ya watoto wao kudaiwa kupotea kutokana na hofu, ambapo baadhi ya watuhumiwa wamekamatwa wakiwa na visu.



Licha ya wananchi hao kufukuzwa ili kuondoka katika eneo la tukio, bado waliendelea kurusha mawe kwa askari polisi na wanahabari waliokuwepo katika eneo hilo.

Kamanda wa polisi mkoa wa kipolisi Kinodoni Camilius Wambura amesema tukio la mtoto kugongwa ilikuwa haihusiani na kituo cha polisi, lakini kutokana na uchochezi wa watu fulani kituo kimechomwa moto.

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiki amewakumbusha wananchi kuwa wanatakiwa kuwa marafiki wa jeshi la polisi kuliko kuanza uadui usio na msingi hata katika jambo ambalo hawahusiki kwani wahusika wa barabara ni Tanroad na si kituo cha polisi.

Via>>ITV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post