Makubwa Haya!! WAPENZI WAFUNGA NDOA KWA KUTUMIA JENEZA..ANGALIA PICHA HAPA

Stori za watu kutumia jeneza katika shughuli zao mbalimbali zimeendelea kutokea sehemu nyingi duniani..Tuliwahi kuandika stori ya bibi harusi kutumia jeneza kuingia nalo ukumbini na nyingine ilimuhusu mwanafunzi kuingia kwenye mahafali yake akiwa ndani ya jeneza.

Stori nyingine inayofanana na hizo imeingia kwenye headlines leo inatokea Singapore baada ya wapenzi kuamua kufunga ndoa yao huku wakitumia jeneza kama sehemu ya kuongeza mvuto kwenye sherehe yao.Jenny Tay, na Darren Cheng, waliamua kunogesha sherehe yao baada ya kuona ni muhimu kwao kutokana na kufanya kazi ya mazishi kwa muda mrefu na kuamini kifo ni sehemu ya maisha ya binadamu hivyo ni jambo la kawaida kwao.Wamesema pia wameamua kufanya hivyo ili watu wengine waone kifo ni jambo la kawaida na ni sehemu ya kila mmoja kuwa ni lazima atapitia.Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post