Facebook Noma!! BINTI AFARIKI DUNIA AKITUMIA FACEBOOK KWA MUDA MREFU JUANI...Mitandao wa kijamii imeendelea kupata mashabiki wengi duniani na imesaidia kwa kiasi kikubwa kurahisisha mawasiliano baina ya watumiaji wake.

Pamoja na faida tuna zozipata kupitia mitadano kuna wale wengine ambao wamejikuta ikiwadhuru wakiwemo wale ambao hutamani kupata selfie za peke yao ambao wengine imewapelekea kupoteza maisha.

Kuna hii imetokea Romania, ambapo binti wa miaka 14 amepoteza maisha baada ya kukaa juani kwa muda mrefu wakati akitumia mtandao wa Facebook.

Andreea Patuleanu alipoteza maisha baada ya kupata ugonjwa wa kiaharusi uliosababisha apoteze maisha baada ya kukaa juani muda mrefu ili aweze kupata mtandao wa facebook bure.

Polisi wa Romania walisema binti huyo alitumia muda mwingi kukaa juani kabla ya kupoteza maisha ikiwa ni baada ya kushindwa kumudu gharama za kujiunga na mtandao huo kwa kulipia.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post