HII HAPA ORODHA YA MAJIMBO MAPYA 26 YA UCHAGUZI YALIYOTANGAZWA NA NEC




Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu Damian Lubuva (wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati akitangaza majimbo mapya ya uchaguzi katika Ukumbi wa Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam leo.


TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza majimbo 26 mapya ya uchaguzi ambayo yatakuwa na wagombea katika uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 25 mwaka huu.


Akizungumza na waandishi wa habari leo Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu Damian Lubuva amesema kukata kwa majimbo hayo wamezingatia idadi ya watu pamoja na Jiografia katika majimbo mapya.
Amesema katika upande wa Zanzibar majimbo yamebaki kuwa 50 kama awali hiyo inatokana vigezo vilivyowekwa na tume hiyo.


Majimbo yaliongezwa ni Handeni Mjini, Nanyamba, Makambako, Butiama, Tarime Mjini, Tunduma, Msimbo, Kavu, Geita Mjini, Mafinga Mjini, Ushetu, Nzega Mjini, Kahama Mjini, Kondoa Mjini, Newala Mjini, Bunda Mjini, Mbulu Mjini, Ndanda, Madaba, Mbinga Mjini, Mbagala, Kibamba,Vwawa,Monongo,Mlimba, Pamoja na Uliambulu.


Jaji Lubuva amesema baadhi ya wabunge wamekuwa wakiingia katika Halmashauri mbili hiyo kuweka mipaka katika maeneo ili mbunge aweze kushiriki katika Halmashauri moja tu.
Amesema baadhi majimbo yamebadilishwa majina na kuendelea kuwepo kwa majimbo hayo kisheria.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post