WATALII WAVUA NGUO NA KUPIGA PICHA ZA UCHI JUU YA MLIMA,WAKIONA CHA MOTO

478

Kuna wakati watu wengine sio kwamba hawapendi watalii au hawapendi utalii kwenye nchi yao, Utalii unakuja na vingi ikiwemo utamaduni mgeni.. Ukiwa maeneo ya Beach hivi kukutana na Watalii wakiwa na nguo ndogo  ndogo (za ndani) huku wakipunga upepo ni kawaida tu, lakini kwa wengine hiyo sio sawa!!

Watalii wanne wamejikuta wakiingia kwenye Headlines za vyombo vikubwa vya Habari Duniani kama Sky News, BBC na CNN.. ishu ni kitendo cha Watalii hao kuvua nguo wakati wanatalii juu ya Mlima Kinabalu ulioko Malaysia, alafu wakapiga picha wakiwa hawajavaa nguo kabisa !!

Mwongozaji wa Watalii hao aliwaambia lakini kwamba ishu ya kuvua nguo sio poa kabisa kwa Malaysia na Sheria zao, majibu yao hayakuwa mazuri>>> “shut up” and “go to hell“.

Jamaa hao walianza kama utani yaani kutaniana nani ataweza kuvua nguo alafu wapige picha, matokeo yake wote wanne wakavua.. Mitandao ikakuza story mwisho wake kesi yao inaendelea Mahakamani.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post