KUHUSU MWANAMME ALIYEKATWA UUME WAKE NA KUPEWA MWINGINE


Daktari wa upasuaji nchini Afrika Kusini amethibitisha kwamba mwanamme wa kwanza aliyepandikizwa uume atakuwa baba hivi karibuni.

Professor Andre van der Merwe, ambaye ndiye aliyefanya upasuaji huo mwezi Disemba, amesema mwenza wa mgonjwa huyo ana uja uzito wa miezi minne.

Mwanamme huyo mwenye umri wa miaka 21 alipoteza uume wake pindi alipokuwa anafanyiwa tohara ambayo haikufanikiwa.

Professor van der Merwe ameendelea kusema habari hizo zinaonyesha kuwa upandikizwaji huo wa kiungo umefanikiwa kabisa na unaweza kufanyiwa wagonjwa wengine katika siku zijazo.

Via>>BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post