YANGA VETERANI WAICHAPA SIMBA VETERANI 3-2 MCHEZO WA KUCHANGIA ALBINO SHINYANGA

Mchezo wa Hisani kati ya wakongwe wa soka  wa  Timu ya Simba na Yanga ulioandaliwa na taasisi ya Mzalendo Foundation kwa lengo la kupata pesa kusaidia watoto wenye ulemavu wa ngozi(albino) katika kituo cha Buhangija kilichopo katika manispaa ya Shinyanga umefanyika jana jioni katika Uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga kwa maveterani wa Yanga kuibamiza Simba Veterani bao 3-2. Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog


Yanga Veterani walijipatia bao la kwanza katika dakika ya pili kipindi cha kwanza kupitia kwa mchezaji wao Deo Lukasi na katika dakika 21 Ally Yusuph akaiongezea Yanga bao la pili.
 
Katika dakika ya 17 kipindi cha pili Simba Veterani wakajipatia bao la kwanza kupitia kwa Shauri Idd na dakika ya 19 kipindi cha pili Deo Lukasi wa Yanga Veterani akaongeza bao la tatu na katika dakika ya 23 kipindi cha pili Monja Liseki akaipatia Simba bao la pili.
Watoto wenye ulemavu wa ngozi kutoka kituo cha Buhangija wakiangalia mechi kati ya Yanga Veterani na Simba Veterani katika uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga

Mashabiki wa soka mkoa wa Shinyanga wakiangalia mpambano huo ambao haukuwa na kiingilio bali mchango wowote kuanzia shilingi elfu moja kwa ajili ya kuwasaidia watoto wenye ulemavu wa ngozi katika kituo cha Buhangija katika manispaa ya Shinyanga.

Wakazi wa Shinyanga wakiwa katika uwanja wa CCM Kambarage

Wakazi wa Shinyanga wakiwa katika uwanja wa Kambarage


Wachezaji wa Simba Veterani wakiwa na  baadhi ya watoto wenye ulemavu wa ngozi wanaolelewa katika kituo cha Buhangija mjini Shinyanga.

Wachezaji wa Yanga Veterani wakiwa na  baadhi ya watoto wenye ulemavu wa ngozi wanaolelewa katika kituo cha Buhangija mjini Shinyanga.


Wachezaji wa Yanga Veterani wakiwa na  baadhi ya watoto wenye ulemavu wa ngozi wanaolelewa katika kituo cha Buhangija mjini Shinyanga.

Mwenyekiti wa taasisi ya Mzalendo Foundation inayojihusisha na Utawala Bora,Haki za binadamu,utamaduni na michezo Khamis Mgeja akiwa na waamuzi wa mchezo huo pamoja na viongozi mbalimbali wa CCM
Mwenyekiti wa taasisi ya Mzalendo Foundation inayojihusisha na Utawala Bora,Haki za binadamu,utamaduni na michezo Khamis Mgeja akiwa na waamuzi wa mchezo huo pamoja na viongozi mbalimbali wa CCM na watoto wenye ulemavu wa ngozi kutoka kituo cha Buhangija
Mwenyekiti wa taasisi ya Mzalendo Foundation inayojihusisha na Utawala Bora,Haki za binadamu,utamaduni na michezo Khamis Mgeja akizungumza katika uwanja wa CCM Kambarage ambapo alisema taasisi yake imeandaa mchezo huo ili kupata pesa kwa ajili ya kununua mahitaji wanayohitaji watoto wenye ulemavu wa ngozi katika kituo cha Buhangija.
Mgeja alisema pesa zote zilizopatikana katika mchezo huo zitakuwa kwa ajili ya watoto wenye ulemavu wa ngozi katika kituo cha Buhangija.

Bwana Peter Bubinza mkazi wa Shinyanga ambaye ni mlemavu wa ngozi akizungumza uwanjani ambapo aliwataka watanzania kuachana na imani potofu kuwa viungo vya albino vinaleta utajiri kwani ingekuwa ni kweli basi maalbino wote wangekuwa matajiri.
Mc maarufu kutoka mkoa wa Shinyanga Ice akiwa na mshangaliaji wa Yanga .
Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post