WABUNGE WAAGA MWILI WA MBUNGE ALIYEFARIKI AKIWA USINGIZINI HUKO DODOMA,MTUMISHI WA MUNGU AWATAKA KUACHA USHIRIKINA!

Simanzi vilio na majonzi vimetanda katika viwanja vya bunge wakati mwili wa aliyekuwa mbunge wa Ukonga Mh Eugene Mwaiposa ulipokuwa ukiwasili katika viwanja vya bunge mjini Dodoma kwa ajili ya waheshimiwa wabunge na watu mbalimbali kutoa heshima za mwisho kabla ya kusafirishwa kupelekwa jijini Dar es Salaam kwa mazishi.


Mwili huo uliwasili ukitokea katika hospitali ya mkoa wa Dodoma ulipokuwa umehifadhiwa ambapo akitoa salamu za bunge Mh Naibu spika Job Ndugai amesema marehemu alikuwa ni miongoni mwa wabunge wa jimbo ambao walikuwa ni mahiri.


 
Naye mchungaji Samweli Mshana kutoka katika kanisa la kiinjIli la kilutheri dayosisi ya Dodoma amewataka wabunge kusimama katika imani zao na kumtegemea mungu na siyo kujiingiza katika mambo ya kishirikina.


 
Akitoa shukrani za familia shemeji wa marehemu Bw Karim Mtambo amesema wanashukuru kwa kila jambo lilofanyika ila jambo kuu wanaiomba bunge katika kumuenzi marehemu watekeleze kwa vitendo yale aliyokuwa akiyasimamia bungeni.


 
Baadhi ya wabunge akiwemo Mh Iddy Azzani na Mh  Hilary Aeshi wamesema marehemu alijitahidi kupinga ufisadi na hasa ubinafishwaji wa shirika la usafiri UDA ambao ulifanyika bila ya kufuata taratibu huska pia alikuwa nguzo muhimu katika kamati yake ya Tamisemi.


 
Mh Mwaiposa alikuwa mbunge wa jimbo la Ukonga (CCM) ambaye alifariki dunia siku ya jumanne tarehe mbili kwa shinikizo la damu nyumbani kwake mjini Dodoma eneo la Chaduru na ameacha mume na watoto wawili.

Via>>ITV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post