SAFARI YA NDEGE YAAHIRISHWA BAADA YA NYUKI KUVAMIA

bee 

Nyuki waliwahi kuibua stoty kubwa baada ya kuvamia ndege aina ya Boeing 757 mwaka 1996 ambapo ndani ya dakika tano baada ya kuondoka ilikuwa ishu baada ya kugundulika kwamba sehemu ambayo inaonesha mwendokasi wa ndege imezibwa na kundi la nyuki.

Leo kuna hii stori kutoka Uingereza inayohusisha nyuki na ndege.. abiria walilazimika kukaa kwa masaa mawili baada ya nyuki kuingia kwenye moja ya mitambo ya injini za ndege, haikuwa salama sana ndege hiyo kuanza safari wakati kuna hali hiyo.

Ndege hiyo inayoitwa Flybe yenye namba BE384 ilikuwa ikitoka Southampton kuelekea Dublin.
Shirika linalomiliki ndege hiyo limesema isingekuwa salama sana wao kuendelea na safari wakati nyuki wako ndani ya injini, ilibidi watolewe na baadae safari yao ikaendelea..

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post