Noma Sana!! ANGALIA PICHA 6 ZA JUMBA MATATA LA MCHEZAJI ASAMOAH GYAN LENYE THAMANI YA BIL 6


 

Asamoah Gyan ni mmoja wa wachezaji wanaolipwa vizuri kutoka katika bara la Afrika, na hakuna uthibitisho mzuri wa kuonyesha ukubwa malipo yake zaidi ya ili hii mali mpya alionunua, jumba kubwa la kifahari.

Mshambuliaji wa Klabu ya Al Ain ambaye analipwa kiasi cha $200,000 kwa wiki amenunua jumba hilo lenye thamani inayokadiriwa kufikia dola millioni 3 za kimarekani ambazo zinafikia billioni 6 za kitanzania.

Jumba hilo lipo maeneo ya McCarthy Hills enclave jijini Accra lina baa mbili, bwawa kubwa la kuogelea. Lina ghorofa tatu zilizotengenezwa kwa muundo wa kipekee kila mmoja huku vifaa vya ulinzi vikiwa vya kisasa ikiwepo milango na madirisha yenye bullet proof.

Kwa mujibu taarifa za vyombo vya habari vya Ghana, Gyan aliinunua nyumba hiyo aliyoikarabati alipozuru nchini humo mwezi April wakati alipoenda kutazama pambano la masumbwi kati Emmanuel Tagoe na Jobert Delos Reyes.



Bwawa la kuogelea



Sehemu ya Ndani ya Nyumba hiyo


Sebule ya Nyumba hiyo


Inavyoonekana kwa Nje Nyumba hiyo


Mojawapo ya vyumba vilivyopo ndani ya Jumba hilo


Sehemu ndogo ya Jiko

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post