PROFESA LIPUMBA ATANGAZA NIA YA KUGOMBEA URAIS TANZANIA

Mwenyekiti wa umoja wa vyama vinavyounda UKAWA nchini na mwenyekiti wa chama cha wananchi (CUF) Mhe. Prof Ibrahim Haruna Lipumba ametangaza nia ya kupeperusha bendera ya ukawa kwa  kugombea urais, katika uchaguzi mkuu ujao Oktoba ili kupewa ridhaa na wananchi ya kuiongoza nchi ya Tanzania.


Akiwahutubia umati mkubwa wa wananchi katika viwanja vya Mwananchi Squer katika mji mdogo wa Urambo mwenyekiti wa UKAWA Ibrahimu Lipumba amesema kuwa, kama UKAWA utaamua kumpitisha mgombea mwingine atakuwa tayari kumpigia debe mteule wa UKAWA, lakini malengo yake ya kutaka kugombea urais, kwalengo la kutafuta haki ya wananchi ambayo imepotea.
 
 
 
Aidha katika hatua nyingine Mhe Prof Ibrahimu Lipumba amewataka watanzania kutambua kwa changamoto ambazo zinawakabili zikiwa ni upatikanaji wa haki za kijamii, zitaondolewa na rais ambaye atatoka nje ya chama cha mapinduzi na si vinginevyo, na kama hawatachagua rais kutoka nje ya CCM wajue hali ngumu ya maisha itaendelea kuwakabili kutokana na kutokuwepo na haki.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post