Makubwa Haya!! WANAWAKE WAFANYA MAANDAMANO WAKIWA UCHI KABISAA

 
Wanawake katika kijiji kimoja cha kaskazini mwa Uganda wamefanya maandamano wakiwa uchi kutokana na mgogoro wa ardhi kati ya utawala wa eneo hilo na jamii ambao umeendelea kwa takribani miaka 10.

 
Wakati wa maandamano hayo ,mawaziri wa serikali na watafiti walipanga kukata kipande cha ardhi katika kijiji cha Apaa huko Amuru.

Utawala wa wanyama pori nchini Uganda unaamini kwamba watu wanavamia ardhi ya uhifadhi wa wanyama pori huku wakazi wakidai kwamba ardhi hiyo ilikuwa ya mababu zao.

Mwandishi wa BBC anasema kuwa katika kabila la Acholi ,mwanamke anapovua nguo na kusalia uchi ni zaidi ya kupigana kwa kuwa inatoa laana kwa mpinzani wake.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post