ASIYEMPENDA LOWASSA AKALE LIMAO__ASKOFU GWAJIMA


Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Askofu Josephat Gwajima amesema kwamba mwananchi  au mwanasiasa  yeyote asiyempenda Mbunge wa Monduli Edward Lowassa akale limao.

Askofu Gwajima alisema hayo juzi  mara baada ya Edward Lowassa kumaliza hotuba yake wakati akitangaza  nia ya kutaka kugombea  urais katika uchaguzi mkuu kwa  tiketi  ya  Chama cha Mapinduzi, CCM.

Kabla ya kumaliza hotuba yake wananchi walimshinikiza Edward Lowassa amsimamishe Askofu Gwajima  ndipo Lowassa alimuita na kumpa maiki aongee na wananchi waliofurika katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid  jijini Arusha.

Askofu Gwajima  alianza kwa kuomba mwenyezi Mungu aibariki safari ya Matumaini ya Mbunge wa Monduli Edward Lowassa na mwisho kabisa kuwapa mjumbe mzito wananchi kuwa mwenye Chuki na Lowassa akale limao.
 
 Via>>Kibonajoro

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post