Maskini!! MWANAMKE HUYU AMWAGIWA MAFUTA YA MOTO USONI NA MKE MWENZA!!!


Wakati chama cha waandishi wa habari wanawake(TAMWA) kikilaani ukatili katika jamii mwanamke mmoja mkazi wa Sokoine Road mjini Songea mkoani Ruvuma Bi.Rehema Gwaya amefanyiwa ukatili na mke mwenzake kwa kumwagiwa mafuta ya moto usoni na kuungua sehemu mbalimbali  za mwili wake.Bi. Rehema Gwaya ambaye amelazwa katika Hospitali ya mkoa Songea akiwa na mwanae wa miezi saba anasema chanzo cha kufanyiwa ukatili huo ni kutofautiana na mke mwenzake aitwaye Zefania Chimgege baada ya kuhoji masuala ya usafi ambapo Zefania aliyekuwa akipika maandazi akamwagia karai la mafuta ya moto usoni.


Baada ya kufanyiwa unyama huo shemeji yake ambaye ni mume wa Zefania Bw.Hafidh Hamidu Mbaya akamwambia atoke nje ammalizie kwa kumchoma na kisu.


Mganga mfawidhi katika hospitali ya mkoa Songea(HOMSO) Dkt.Benedikt Ngaiza amesema amempokea  mgonjwa huyo 

Wakazi wa Songea wamelaani ukatili huo.

Rehema Gwaya na Zefania Chimgege wameolewa sehemu moja na wote wanaishi katika nyumba ya baba Mkwe na waume zao na kwamba Zefania Chimgege anashikiliwa na polisi kwa kufanya ukatili huo.

Via>>ITV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post