Duh!! MCHEZAJI AKIONA CHA MOTO BAADA YA KUMSHIKA SHIKA MAKALIO MWENZIE UWANJANI
Ligi ya Copa America ni moja ya Ligi za soka ambazo ni maarufu sana duniani, lakini headlines mfululizo ndani ya wiki moja sasa hivi sio stori nzuri sasa.. tulisikia kuhusu Shirikisho la Soka Amerika ya Kusini kumpa adhabu ya kusimamishwa mechi nne staa wa soka toka Brazil ambae pia ni winga wa pembeni katika Kikosi cha Barcelona, Neymar da Silva Santos JĂșnior.

Leo nimempata huyu mwingine Gonzalo Jara ambaye na yeye kaingia kwenye headlines baada ya kumshika mchezaji mwenzake Cavani skwenye makalio.. inaonekana ni kama haikuwa bahati mbaya kwa vile kabla hajamshika kulitokea kujibizana kati yao.. Video ya tukio hilo imeendelea kusambaa mitandaoni kutokana na hukumu kuonekana kumwangukia asiye na hatia.

Edinson Cavani alikasirishwa na kitendo cha Gonzalo, akampiga kibao cha uso.. refa akatoa kadi ya njano kwa Cavani, lakini kwa vile tayari jamaa alikuwa na kadi ya njano ikabidi apigwe nyekundu na kutolewa nje ya uwanja.


Mechi hiyo ilikuwa kati ya Chile na Uruguay.. wachambuzi wanamjadili Gonzalo bado, wanasema ikitokea Uchunguzi ukaonesha jamaa ni kweli alimshika Cavani kwenye makalio hii itakuwa mara ya pili kwake kufanya kosa linalofanana kabisa na alilomfanyia Luis Suarez mwaka 2013, na mwisho ikawa hivyohivyo Suarez kupiga ngumi ya uso.


Unaweza kucheki kilichoendelea hapa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post