Picha_BASI LA " ANOTHER G"LAGONGANA NA LORI NA KUUA WATU ZAIDI YA 20 HUKO IRINGA


Eneo la tukio


Watu  23 wamepoteza maisha  usiku   huu katika ajali ya  gari aina  ya costa mali ya Another G inayofanya  safari  zake kati ya Njombe - Iringa baada ya  kugongana na  Lori/Semi Traille.

 Habari za awali zinasema kuwa ajali hiyo imetokea baada ya basi hilo kukwepa bajaji,na kugongwa na lori.

Taarifa za  awali  ambazo    tumezipata  kutoka  eneo la tukio zinadai kuwa ajali hiyo imetokea  eneo la Kinyanambo nje  kidogo na mji wa Mafinga wilaya ya  Mufindi  mkoani Iringa wakati  gari hiyo ya Another G ikitokea  Njombe  kwenda Iringa.

Inaelezwa kuwa waliofariki dunia mpaka sasa ni 23, majeruhi ni 34.Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post