NIMEKULETEA PICHA NYINGI KUTOKA KWENYE MKUTANO MKUBWA WA CHADEMA MJINI SHINYANGA


Hapa ni katika eneo la Ngokolo Mitumbani mjini Shinyanga ambako leo jioni kumefanyika mkutano mkubwa wa Chadema/UKAWA ukiongozwa na mwenyekiti wa Baraza la Vijana(BAVICHA) Chadema Taifa Patrobas  Katambi na viongozi mbalimbali wa BAVICHA taifa.Lengo la mkutano uliohudhuriwa na maelfu ya wakazi wa Shinyanga ilikuwa ni kutoa elimu ya uraia-picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema katika wilaya ya Shinyanga mjini  Samson akizungumza katika mkutano wakati wa kukaribisha viongozi wa BAVICHA taifa katika mkutano wao uliofanyika katika kata ya Ngokolo mjini Shinyanga.Pamoja na mambo mengine alieleza kutoridhishwa na wabunge wa CCM huku akisisitiza kuwa endapo Gaki ama Stephen Masele watapitishwa kugombea yuko tayari kupambana nao
Meza kuu wakiwa eneo la mkutano
Kushoto ni Mwenyekiti wa BAVICHA mkoa wa Iringa akizungumza katika mkutano ho wa hadhara
Meza kuu wakiwa eneo la mkutano

Wakazi wa Shinyanga wakifuatilia mkutano huo

Wakazi wa Shinyanga wakiwa eneo la mkutano

Msemaji wa BAVICHA Elius Julius akizungumza na wakazi wa Shinyanga

Wakazi wa Shinyanga wakiwa eneo la tukio
Katibu BAVICHA taifa  Mwita Julius akizungumza katika mkutano huo ambapo alieleza kukerwa na utitiri wa wanaccm kuwania urais hali ambayo alisema inaonesha ni kiasi wasivyoaminiana na kuwa na tamaa ya kutafuna pesa za wananchi
Hapa siyo sokoni bali ni katika eneo la mkutano
Tunafuatilia mkutano......
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema Taifa Patrobas  Katambi akiwa na Katibu BAVICHA taifa  Mwita Julius
Wananchi wanafuatilia kinachoendelea kwenye mkutano

Kulia ni Naibu katibu mkuu wa Baraza la Vijana Zanzibar Omary Nassoro akimkaribisha jukwaani mwenyekiti wa BAVICHA taifa Patrobas Katambi ili azungumze na wakazi wa Shinyanga.
Awali Naibu katibu mkuu wa Baraza la Vijana Zanzibar Omary Nassoro aliwatahadharisha watanzania wakati wa uchaguzi mkuu ujao kuchagua viongozi wanaowafaa badala ya kuchagua viongozi wanaojali maslahi yao binafsi.

Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema Taifa Patrobas  Katambi akizungumza katika mkutano huo ambapo
amewataka wanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kuungana pamoja  na kuepuka migogoro ili kuiondoa madarakani serikali ya Chama Cha Mapinduzi badala ya kugombania madaraka ndani ya chama.

Patrobas Katambi alieleza pia nia yake ya kuwania ubunge katika jimbo la Shinyanga mjini na endapo jina lake likikatwa yupo tayari kumpa ushirikiano mgombea wa Chadema kwani CHADEMA inaamini katika umoja na mshikamano


Mwenyekiti huyo wa BAVICHA pia  amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura kwani ndiyo tiketi itakayotumika kuondoa viongozi wasiofaa kwa wananchi.

Mtangaza nia kuwania ubunge katika jimbo la Shinyanga mjini Francis Kasiri akiwasalimia wakazi wa Shinyanga

Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema Taifa Patrobas  Katambi,ambaye pia ni mtangaza nia kuwania jimbo la Shinyanga akiwa amebebwa na wakazi wa Shinyanga baada ya mkutano kuisha
Wakazi wa Shinyanga wakitafakari jambo baada ya mkutano wa CHADEMA kumalizika.

Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post