SENTENSI 23 ZA MHESHIMIWA MWIGULU NCHEMBA AKITANGAZA NIA YA KUWANIA URAIS TANZANIA , MTU ANASTAAFU HALAFU UNAMUONGEZEA MUDA WA NINI WAKATI KUNA VIJANA HAWANA AJIRA

 

Mwigulu: Namshukuru MUNGU kwa kuniwezesha leo kusimama mbele yenu kwaajili ya kutangaza jambo kubwa kwa ajili ya nchi yetu.

Mwigulu: Nimeamua kutangazia nia Dodoma kwakuwa ni Makao makuu ya Nchi na pia makao makuu ya chama.

Mwigulu: Nilipomaliza shahada ya 2 nilibeba zege na mke wangu alipika mama ntilie, natambua tatizo la ajira kwa vijana.

Mwigulu: Kukaa sana serikalini si kigezo, unaweza kukaa sana serikalini na ukawa umesababishia hasara kubwa Taifa hili

Mwigulu: Kiongozi akipatikana kwa mazoea, atafanya kazi kwa mazoea. Nawaambieni tunataka tukomeshe kufanya kazi kwa mazoea.

Mwigulu: Unafanya kazi ukiwa na nguvu na ukimaliza unapumzika, kwahiyo unajiuliza tena hilo?

Mwigulu: Mkataba wa Rais wa awamu ya tano ni juu kazi anazoenda kufanya na sio kazi alizowahi kufanya.

Mwigulu:Mambo ya kuzingatia ni Kila mtu kulipa kodi anayostahili na sio kukandamiza wafanyakazi na kinamama wauza vitumbua.

Mwigulu: Pia jambo lingine la kuzingatia ni Udhibiti wa matumizi mabaya ya fedha na kuacha kufanya kazi kwa mazoea.

Mwigulu: Awamu ya 5 nataka kuona nchi ikiingia kwenye uchumi wa viwanda na vijana wakifanya kazi kwa shift usiku na mchana.

Mwigulu: Rushwa hupofusha macho ya wenye akili na rushwa hurudisha nyuma maendeleo

Mwigulu: Mtu yoyote akithibitika amefanya vitendo vya rushwa, atafilisiwa, atafukuzwa kazi na atafungwa.

Mwigulu: Mtu anabakiza muda mchache hadi anakuja kustaafu unamuongezea muda tena kazini wakati kuna vijana wasio na kazi.

Mwigulu: Ninaposema kukomesha rushwa nitazingatia maslahi ya Wafanyakazi, haiwezekani wengine Wale kidogo na wengine kubwa.

Mwigulu: Mtu anayeiba dawa ambazo zingemtibu maskini huyo ni mhujumu, tutamnyang'anya leseni yake na atakwenda jela.

Mwigulu: Tutasimamia Muungano wetu maana sio wa vitu ila ni watu. tutahakikisha uchumi wa Zanzibar nao utapewa kipaumbele.

Mwigulu: Nawaambieni nawaomba kazi hii nikiwa bado nina nguvu ili niweze kufika mwenyewe maeneo yenye migogoro ya ardhi.

Mwigulu: Ninapotangaza nia ya jambo hili nimetathimini vya kutosha na nikajiridhisha na ahadi yangu ni kwamba nitawavusha.

Mwigulu: Tunaposimamia kuacha kufanya kazi kwa mazoea ndio tunasema mabadiliko ni vitendo na wakati ni sasa

Mwigulu: Ukiwaondoa vijana mjini wakati wakifanya kazi halali kwa kigezo cha uchafu,watarudi mjini na kufanya kazi haramu

Mwigulu: Natangaza rasmi kuomba ridhaa ya kugombea katika chama changu ili niweze kuleta mabadiliko Katika Nchi yangu.

Mwigulu: Napoenda kupigana vita hii siendi kupigana kwaajili ya Watanzania ila mimi mwenyewe maana umaskini unanigusa.

Mwigulu: Mambo matatu ninayowaomba Watanzania ni kwamba mniamini, pili mniunge mkono na tatu nitawavusha.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527