WATANZANIA WATAKIWA KUTHAMINI TIBA ZA ASILI -MITI SHAMBA


Malunde1 blog leo imekutana na katibu mkuu wa taifa wa Chama cha Tiba asili am,baye pia ni mkurugenzi wa Kituo cha Ukombozi Herbal Clinic and Research Centre kilichopo jijini Dar es salaam ,Dkt Issa Ally Njoka maarufu kwa jina la "Mkombozi",akiwa katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga akiwa katika banda lake kwenye maonesho ya viwanda Vidogo kanda ya ziwa.Pichani ni Dkt Mkombozi akielezea matibabu na dawa mbalimbali za asili wanazotoa
Dkt Mkombozi akimuonesha mkazi wa Shinyanga aliyefika katika banda hilo la Tiba za asili,ambapo alisema wanatibu magonjwa mbalimbali sugu ikiwemo Kisukari,Vidonda vya Tumbo,Presha n.k
Dkt Mkombozi akionesha picha ya moyo na kusisitiza kuwa wanatibu maradhi mbalimbali ya moyo.Anasema Tiba asili ni dhahabu ya kijani,na kwamba tiba asili siyo Ushirika ni mama wa tiba za kisasa kwani historia yake ni kongwe tangu enzi za mababu hivyo wote tushirikiane kuiboresha

Dkt Mkombozi akionesha picha za magonjwa mbalimbali 

Dkt Mkombozi aliwataka watanzani akuthamini dawa za asili badala ya kuendekeza mambo ya kigeni kwa kuamini kuwa ni bora zaidi wakati hata dawa zingine za kisasa zimetokana na mitishamba.Anasema ni wakati mzuri sasa kwa watanzania kuthamini utamaduni wao badala ya kuendekeza utamaduni wa kigeni kwa sababu dawa za asili zinatibu kwa haraka zaidi,lakini pia ni vyema kukutana na wataalam wa kweli wa dawa za asili.
 Kama unahitaji matibabu ya magonjwa mbalimbali yakiwemo magonjwa sugu,muone Dkt Mkombozi anayepatikana katika ofisi yake mtaa wa Magomeni Kagera jijini Dar es salaam,au piga simu namba 0784 364256 au 0767364256 au 0715364256


Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post