MGODI WA ALMASI WA MWADUI WAMETULETEA JIKO LA KUTUMIA NGUVU YA JUA!! ANGALIA PICHA




Maonesho ya raha yake,wakati mwingine unaona vitu ambavyo hujawahi kuona tangu uzaliwe….basi Malunde1 blog inakukutanisha na wataalam kutoka mgodi wa almasi wa Mwadui ( Williamson Diamonds Limited) uliopo wilayani Kishapu mkoani Shinyanga ambao wamekuja na Jiko la Kisasa linatumia nguvu ya jua katika maonesho ya Viwanda Vidogo Kanda ya Ziwa yanayoendelea katika Viwanja vya Shycom mjini Shinyanga.






Afisa Usalama,Afya na Mazingira kutoka mgodi wa Mwadui Donatus Mukungu akitoa maelezo juu ya mradi huo wa jiko la kutumia nguvu ya Jua kwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga (mwenye miwani kushoto)aliyetembelea banda la mgodi huo Mei 30,2015.


Afisa Mazingira kutoka Mgodi wa Mwadui Prisca John akionesha yai lililoiva ndani ya dakika 10 baada ya kuwekwa kwenye jiko hilo la kutumia nguvu ya jua


 Afisa Mazingira kutoka Mgodi wa Mwadui Prisca John  akimenya yai
Afisa Usalama,Afya na Mazingira kutoka mgodi wa Mwadui Donatus Mukungu alisema majiko mengine ya namna hiyo yanaendelea kutengenezwa na wana mpanga wa kuanza kuyasambaza jijini 


Mfanyakazi kutoka Mgodi wa Mwadui akiwa amesimama mbele ya jiko hilo la kisasa
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga akiangalia asali iliyotengezwa katika mgodi wa Mwadui
Afisa Usalama,Afya na Mazingira kutoka mgodi wa Mwadui Donatus Mukungu akieleza shughuli mbalimbali zinazofanywa na mgodi wa Mwadui,ambapo alisema wanafanya kazi za kutunza mazingira pia


Wakazi wa Shinyanga wakiwa katika banda la mgodi wa Mwadui katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga


Afisa Mazingira mgodi wa Mwadui(kushoto) akionesha nta iliyotengenezwa katika mgodi huo


Afisa Mazingira mgodi wa Mwadui akiwaeleza wakazi wa Shinyanga namna shughuli za uchimbaji madini zinavyofanyika.
Maonesho ya 13 ya Viwanda Vidogo Kanda ya ziwa yameanza Mei 28 mwezi huu na Kilele chake kitakuwa Juni 2015 ambapo wajasiriamali mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi wanaonesha kazi zao katika Viwanja vya Shycom mjini Shinyanga.

Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527