WAENDESHA DALADALA WA SHINYANGA MJINI WAMEBISHANA SANA LEO,WALICHOKIAMUA NI HIKI!!

Leo katika pitapia za Malunde1 blog tukakutana na kituko hiki!! Waendesha baiskeli mjini Shinyanga maarufu "Daladala" wamebishana sana wakiulizana nani mkali wa kuendesha baiskeli,basi wakachangisha shilingi elfu moja moja kila mmoja walau ifikie shilingi elfu 5 kwa ajili ya mshindi wa kwanza,kweli ikawa hivyo walichokiamua ni kuendesha baiskeli kutoka Nguzo nane hadi Ibinzamata kwa speed ya ajabu.
Wakati wanamalizia mbio zao katika eneo la Nguzo Nane ghafla mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga,Gulam Hafeez Mukadam ambaye ni diwani wa kata ya Shinyanga mjini akakatisha katika eneo hilo na kuona watu wamevua mashati yao na kutaka kujua kulikoni?,Jibu Tunatangaza mshindi wetu!! Tumpe Buku Tano zake!!

Kufuatia kitendo hicho cha kufanya mashindano barabarani akawashauri kufanya mashindano hayo kwa utaratibu unaotakiwa kwani pengine wangesababisha ajali kutokana na barabara waliyotumia kutumiwa na magari,pikipiki,watembea kwa miguu tena bila taarifa kwa vyombo vya usalama barabarani.

"Nawaongeza zawadi kwa shindano lenu hili,lakini hamjafuata utaratibu,siku nyingine mtoe taarifa na mfanye kwenye eneo salama,najua mnapenda michezo na baiskeli mnazipenda mnachotakiwa ni kufuata utaratibu ndugu zangu",alisema Mukadam

Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post