SIMBA WAZEE NOMA- WATAFUNA MBUZI ZAIDI YA 20 ,WATEMBEA USIKU KUKIONA CHA MOTO


Wananchi katika kijiji cha Matemanga wilayani Tunduru mkoani Ruvuma wanaishi kwa hofu na kulazimika kutotembea usiku wakihofia kuliwa na simba wanaosumbua katika kijiji hicho  wakidaiwa kutoroka katika hifadhi ya taifa ya  Selou  ambapo  mpaka sasa wameshakula mbuzi  zaidi ya ishirini.


Wamesema simba hao wanaodaiwa kuwa watatu na wazee ambao inadaiwa wametoroka porini baada ya kushindwa kuwinda kutokana na uzee tayari  wameshakula mbuzi zaidi ya ishirini kijijini hapo.

Wamesema simba hao wamekuwa wakisumbua katika kijiji hicho nyakati za usiku  na kuwafanya waishi kwa hofu  wakihofia kuliwa na simba hao.

Mhifadhi wa wanyamapori katika wilaya ya Tunduru Charles Shawa  anasema  msako mkali wa kusaka simba unaendelea huku akisema ni simba mmoja  tu ndiye  anayesumbua  kijijini hapo.

Mkuu wa wilaya ya Tunduru Chande Bakary Nalicho anasema nguvu zimeongezwa katika msako wa simba  ambapo kuna askari wanyamapori sita katika  msako wa simba.
Via>>ITV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post