NIWEKUWEKEA PICHA ZA BEHIND THE SCENE FILAMU YA KIMATAIFA "BINTI KIBENA"



Chozi la Binti Kibena,ni filamu ya Kitanzania yenye lengo la kufichua vitendo vya kikatili vinavyofanywa kwa watoto hususani wa kike, mfano wa vitendo hivyo kama vile unyanyasaji wa kijinsia,ubakaji,ndoa za utotoni na vingine vingi.
Maudhui ya Filamu hii kwa kiasi kikubwa yamejikita katika kukemea ndoa za utotoni ambapo vyanzo mbalimbali vya ndoa za utotoni,athari na madhara anayoyapata mtoto anayeolewa angali mdogo vimebainishwa.
Filamu ya Chozi la binti Kibena imeandikwa na Amani Masuka na 
kutayarishwa na Dr. Monica Muhoja Edutaiment Centre (MOMEC),mpiga picha akiwa ni Amani Masuka,
na kuhaririwa na Amani Masuka na Baraka Makaba
na Muongozaji ni Dennis Sweya (Dino).
Ndani ya filamu ya CHOZI LA BINTI KIBENA utakutana na Kisa cha kusisimua chenye kuhuzunisha,kufundisha na kuburudisha kinachomuhusu Tunu,(Binti Kibena).

Pia Utakutana na wasanii wakongwe kama Riyama Ally, Dennis Sweya Dino, Lutwaza Philmon (The Next Kanumba) Nassoro Ndambwe nk.
Pia  filamu hii imeibua vipaji vipya kama Maria Sweya (Tunu) alie vaa uhusika mkuu na kufanya mambo makubwa kiasi ambacho kilimshangaza Riyama Ally aliyecheza naye kama mama yake wa kufikia.

Wengine ni Bity,Tid Clever,Irene Kitaa,Gema Isack,Hans Chamoto nk.
Filamu hiyo ya Kihistoria imeshakamilika kinachosubiriwa sasa ni tarehe rasmi ya uzinduzi,ambapo watanzania watapata wasaa mzuri kabisa wa kuiona kwenye jumba la sinema kisha mtaani.
MOMEC inawashukuru wadau wote walio iwezesha filamu hiyo kukamilika katika ubora wa kimataifa na inawaomba watanzania kuipokea kwa mikono miwili kwani watapata kitu ambacho kitakata kiu yao ama kitawapa mtazamo mpya wa level za kimataifa.
TAZAMA BAADHI YA PICHA KATIKA FILAMU HIYO HAPA CHINI




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post