MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA WAKUTANA NA WADAU WA AFYA MKOANI SIMIYU

Hapa ni katika ukumbi wa Mtakatifu John uliopo mjini Bariadi katika mkoa wa Simiyu ambapo leo kumefanyika semina juu ya Uhamasishaji kuhusu Utaratibu wa Utoaji Mikopo ya Vifaa tiba,Ukarabati wa Majengo na Dawa kwa Vituo vya kutolea huduma za matibabu.Semina hiyo imeandaliwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya( National Health Insurance Fund-NHIF) kwa kushirikiana na uongozi wa mkoa wa Simiyu.Semina hiyo imehudhuriwa na wadau mbalimbali wa afya kutoka mkoani humo-Picha zote na Kadama Malunde-Simiyu


Mgeni rasmi ambaye ni Katibu tawala msaidizi utawala na rasilimali watu mkoa wa Simiyu ndugu Magohu Zonzo akifungua semina hiyo kwa niaba ya  katibu tawala wa mkoa wa Simiyu.Pamoja na mambo mengine alisema changamoto kubwa katika vituo vingi vya kutolea huduma za afya ni dawa hivyo uwepo wa mikopo kutoka NHIF utakuwa mwarobaini wa changamoto hiyo huku akiwataka wataalam wa afya kuunga mkono NHIF kwa manufaa ya watanzania wote.
Afisa Mkuu wa Udhibiti Vihatarishi vya Malengo kutoka Bima ya Taifa ya Afya kutoka Makao Makuu ndugu Thadeus Machume akizungumza katika semina hiyo ambapo alisema thamani ya mikopo inayotolewa na NHIF inategemea madai ya wastani ya mwezi ya kituo kwa huduma zitolewazo kwa wanachama wa NHIF na kwamba kwa kutegemea na aina ya mkopo,marejesho yatafanyika kila mwezi kwa kipindi chote cha mkopo
Afisa Mkuu wa Udhibiti Vihatarishi vya Malengo kutoka Bima ya Taifa ya Afya kutoka Makao Makuu ndugu Thadeus Machume alisema Riba itakayotozwa katika mikopo yote itakuwa ni bei ya soko,yaani mkopo utatozwa riba ya asilimia moja( 1%) zaidi kutoka kiasi cha riba inayoweza kupatikana kutoka katika uwekezaji wa dhamana za serikali.

Kulia ni kaimu mganga mkuu wa mkoa wa Simiyu Dkt Bahame mteremko akifuatilia kwa umakini zaidi kilichokuwa kinajiri ukumbini
Aliyesimama ni Afisa Mdhibiti Ubora wa Afya kutoka ofisi za Bima ya Taifa ya Afya mkoa wa Shinyanga Dkt Gustav Kisamo ambapo aliwataka wadau wa afya kuchangamkia mikopo inayotolewa na NHIF

Afisa Mdhibiti Ubora wa Afya kutoka ofisi za Bima ya Taifa ya Afya mkoa wa Shinyanga Dkt Gustav Kisamo alisema kutokana na changamoto ya kupotea kwa mapato katika vituo vya afya,mfumo wa kompyuta utafungwa katika vituo ili kuleta ufanisi zaidi.Alisema wamebaini kuwa katika vituo vingi kuna kadi nyingi feki za NHIF na wakati mwingine kutokana na kukosa umakini kwa baadhi ya wataalam wa afya  kadi zinazotumika ni zile zilizoisha muda wake wa matumizi na wakati mwingine wagonjwa kutumia kadi za ndugu zao
Afisa Mkuu wa Udhibiti Vihatarishi vya Malengo kutoka Bima ya Taifa ya Afya kutoka Makao Makuu ndugu Thadeus Machume akiwasilisha mada kuhusu Utaratibu wa Utoaji Mikopo ya Vifaa tiba,Ukarabati wa Majengo na Dawa kwa Vituo vya kutolea huduma za matibabu kupitia NHIF.

Wadau wakifuatilia mada- Afisa Mkuu wa Udhibiti Vihatarishi vya Malengo kutoka Bima ya Taifa ya Afya kutoka Makao Makuu ndugu Thadeus Machume ambaye alisema ili kuondoa tatizo la upatikanaji wa dawa na vitendanishi katika vituo vya kutolea huduma,NHIF imeanzisha mpango wa utoaji mikopo iliyoidhinishwa kuanza kutolewa katika mwaka wa fedha 2014/15. Alisema wasambazaji chini ya programu hiyo watachaguliwa na mfuko ambapo bohari ya madawa(MSD) kama wakala wa serikali watapewa kipaumbele.

Wa kwanza kushoto ni Afisa Mdhibiti Ubora wa Afya kutoka ofisi za Bima ya Taifa ya Afya mkoa wa Shinyanga Dkt Gustav Kisamo,katikati ni mgeni rasmi Katibu tawala msaidizi utawala na rasilimali watu mkoa wa Simiyu ndugu Magohu Zonzo,kushoto kwake ni mwenyekiti wa halmashauri ya mji Bariadi ndugu Robert Rweyo


 Afisa Mkuu wa Udhibiti Vihatarishi vya Malengo kutoka Bima ya Taifa ya Afya kutoka Makao Makuu ndugu Thadeus Machume alisema mpango wa mkopo wa dawa na vitendanishi utaanza kwa majaribio ya miezi sita kwa mikoa 9 ambayo ni Dodoma,Lindi,Pwani,Iringa,Kigoma,Katavi,Shinyanga,Kagera na Manyara.Baada ya kipindi cha majaribio kuisha,mikopo hiyo itatolewa kwa mikoa yote nchini kulingana na matokeo ya taarifa ya majaribio
Aliyesimama ni mwenyekiti wa halmashauri ya mji Bariadi ndugu Robert Rweyo akizungumza katika semina hiyo ambapo aliwataka wataalam wa afya kuwahamasisha wananchi wajiunge na mfuko wa NHIF.

Hali kadhalika alipongeza mpango wa NHIF kufunga mfumo wa kompyuta katika vituo vya afya ili kuleta ufanisi katika ukusanyaji wa mapato
Dkt John Mkinga ambaye ni Daktari msaidizi katika kituo cha Afya cha Muungano mkoani Simiyu akichangia mada katika semina hiyo

Mratibu wa Bima ya Taifa ya Afya halmashauri ya mji wa Bariadi Jahula Method akichangia mada katika semina hiyo
Wadau wa afya mkoani Simiyu wakifuatilia kilichokuwa kinajiri ukumbini
Mhasibu wa NHIF mkoa wa Shinyanga bwana Amiri Abdallah akizungumza katika semina hiyo
BOFYA HAPA KUONA SEMINA YA NHIF MKOANI SHINYANGA

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post