AJALI YA BAJAJI NA LORI YAUA MWENDESHA BAJAJI HUKO NZEGA


Ajali za barabarani zimeendelea kupoteza maisha ya Watanzania ambapo leo asubuhi
Mwendesha bajaji aliyejulikana kwa jina la Hussein Masha mkazi wa Nzega Ndogo wilayani Nzega mkoani Tabora amefariki dunia baada ya kugongwa na gari aina ya Tipa.


Mashuhuda wa ajali hiyo wameiambia Malunde1 blog kuwa mwendesha bajaji huyo alikuwa anatoka Nzega Ndogo kuelekea Nzega mjini ,alipofika katika eneo la Kitongo akataka kukata kona kuingia barabara ya posta ndipo tipa lililokuwa nyuma yake likagonga na kusababisha kifo chake papo hapo huku mwenye tipa akikimbia

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post